Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kushoto), akimsikiliza kwa makini Msanii Wastara Issa (aliyeketi chini), alipokuwa akimweleza namna mguu wake huo, unavyomuuma na ni kwa muda gani amekuwa akisumbuliwa na tatizo hilo jana alipomtembelea nyumbani kwake Tabata Sanene, jijini Dar es Salaam, kumjulia hali na kufahamu ni kiasi gani cha pesa bado kinahitajika kumwezesha kwenda kwenye matibabu yake nchini India. Wa kwanza kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi Joyce Fissoo.(Picha zote na Anitha Jonas – WHUSM)
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kulia) akitoa wito kwa watanzania kujitokeza kumchangia msanii wa filamu Wastara Issa ili aweze kupata matibabu ya mguu wake huko nchini India alipomtembelea msanii huyo nyumbani kwake jana Tabata Sanene jijini Dar es Salaam, na wa kwanza kushoto ni Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa Bw.Godfrey Mngereza na anayefuata ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fissoo, na aliyeketi chini ni Msanii huyo wa Filamu Wastara Issa.
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fissoo (kushoto) akimkabidhi mchango Msanii wa Filamu Wastara Issa aliyeketi chini kiasi cha shilingi milioni moja kilichotolewa na Bodi ya Filamu Tanzania kwa Kushirikiana na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), kitakacho msaidia kwa matibabu ya mguu wake walipomtembelea jana nyumbani kwake Tabata Sanene jijini Dar es Salaam kumjulia hali. Katikati ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akishuhudia tukio hilo.
Na Anitha Jonas – WHUSM
20/01/2018
Dar es Salaam.
WAZIRI wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa wito kwa Watanzania kujitokeza kumchangia msanii wa Filamu Wastara Issa ili aweze kwenda kupatiwa matibabu ya mguu wake unaomsumbua nchini India.
Mheshimiwa Mwakyembe ametoa wito huo alipokwenda kumtembelea msanii huyo wa filamu nyumbani kwake leo Tabata Sanene jijini Dar es Salaam kutokana na msanii huyo kuwa anasumbuliwa na mguu wake uliyokatwa mpaka kufikia kuhitajika kufanyiwa upasuaji mwingine.
“Ndugu zangu watanzania najua kutoa ni moyo na siyo utajiri ninawaomba mjitokeze kwa kumsaidia msanii huyo kwani mpaka sasa anahitaji kiasi cha milioni kumi na nane kwa ajili ya kufanikisha safari yake hiyo ya kwenda kupata matibabu na anatarajia kwenda kwenye matibabu hayo mwezi ujao,”Dkt.Mwakyembe.
Naye Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi.Joyce Fissoo alitoa wito kwa wasanii wote wa filamu nchi kujitokeza na kumsadia mwanatansia mwenzao wa filamu katika kufanikisha anapata matibabu ili aweze kurudi na kuendelea kufanya kazi zake kama kawaida .
“Bodi ya Filamu nchini kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa laTaifa tumetoa kiasi cha shilingi Milioni moja kwa ajili ya kumchangia katika kufanikisha safari yake ya matibabu na serikali kwa ujumla inafanya jitihada mbalimbali katika kuhakikisha msanii huyu anapata kiasi hicho cha pesa kilichobakia,”Bibi Fissoo.
Pamoja na hayo Katibu Mtendaji BASATA Bw.Godfrey Mngereza alitoa wito kwa wasanii wote nchini kwa nao kijitokeza kumchangia msanii huyo kwani wasanii wote ni wamoja kwa maana wote ni wanafanya kazi ya sanaa hivyo ni vyema kuwa na mshikamano na kusaidiana.
Kwa upande wa msanii Wastara Issa aliishukuru serikali kwa kumtembelea na kumjulia hali pamoja na kumchangia na kusema imekuwa nifaraja kubwa kwake kuwaona na alitoa akaunti namba anayotumia kwa ajili ya kukusanyanyia michango ambayo ni EQUITY BENKI – 3007111415583 na namba za simu anazotumia kuchangisha ni 0768 – 666 113 na 0713 666 113 na alieleza amesajiliwa kwa jina la Wastara Issa katika namba hizo za simu pamoja na akaunti namba yake.
No comments:
Post a Comment