Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akiwasisitiza watanzania kuendelea kumwombea Mheshimiwa Rais kama jinsi amekuwa akiwaomba mara kwa mara katika mkutano wa maombi ya kuombea Taifa la Tanzania uliyoandaliwa na kanisa la Abundant Blessings Center jana jijini Dar es Salaam. Aliyeketi kushoto ni Askofu wa Kanisa hilo Flaston Ndabila.
Askofu David Mwansoka wa Kanisa la Abundant akiongoza maombi ya kuliombea Taifa la Tanzania kwa watu waliyojitokeza kushiriki mkutano huo (hawapo pichani) jana jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt.Harrison Mwakyembe na wa kwanza kushoto Mkuu wa Wilaya Kibaha Asumpta Mshama wakifuatilia maombi hayo.
Askofu wa Kanisa la Abundant Flaston Ndabila akimweleza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kushoto) namna kanisa hilo limekuwa na utaratibu wa kuombea Taifa katika mkutano wa kuliombea taifa la Tanzania na viongozi wake uliyofanyika jana jijini Dar es Salaam,wa kwanza kushoto ni Askofu David Mwansoka wa Kanisa hilo.
Waumini wa Kanisa la Abundant wakiwa katika maombi ya kuliombea Taifa la Tanzania yaliyokuwa yakiongozwa na Askofu David Mwansoka (hayupo pichani), jana jijini Dar es Salaam ambapo Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) alikuwa mgeni rasmi.(Picha zote na Anitha Jonas – WHUSM)
No comments:
Post a Comment