TANGAZO


Sunday, January 21, 2018

Australian Open: Nadal afuzu kwa robo fainali baada ya kumshinda Schwartzman

Nadal

Haki miliki ya pichaEPA
Image captionUshindi wa pekee wa Rafael Nadal katika Austalian Open ulikuwa ni mnamo 2009
Rafael Nadal amesogea hadi katika robo fainali za mashindano ya Australian Open kwa kumtimua MuArgentina Diego Schwartzman kwa seti nne.
Nadal, mwenye umri wa miaka 31, alishinda kwa seti 6-3 6-7 (4-7) 6-3 6-3 katika uwanja wa Rod Laver na kufanikiwa kufuzu kupambana na MCroatia Marin Cilic.
Schwartzman, alidhihirisha kuwa mpinzani hodari wa Nadal kufikia kiwango hichi , kwa kufanikiwa kushinda seti ya kwanza ya mashindano hayo dhidi ya bingwa huyo mara 16 wa mshindano ya Grand Slam.
Lakini Nadal alidhihirisha umahiri wake katika seti mbili za mwisho na kushinda katika muda wa saa 3 na dakika 51.
"Ulikuwa ni mpambano mkali. Ni rafiki yangu mzuri," alisema Nadal
"ni mchezaji mahiri, katika nyanja zote, na kwa mara nyingi nilihisi alionyesha mchezo mzuri."
Cilic wa kutoa Croatia alijinyakulia nafasi hiyo katika robo fainali kwa ushindi wa seti 6-7 (7-2) 6-3 7-6 (7-0) 7-6 (7-3) dhidi ya Mhispania Pablo Carreno Busta.

No comments:

Post a Comment