Mchezaji wa kiungo cha kati wa timu ya Manchester United Henrikh Mkhitaryan amekubali kujiunga na timu ya Arsenal, huku Alexis Sanchez akitarajiwa kuhama upande wa pili.
Mkhitaryan, mwenye umri wa miaka 28, ambaye ni raia wa Armenia atafanyiwa ukaguzi wa kimatibabu Leo Jumapili au kesho Jumatatu, huku Sanchez mwenye umri wa miaka 29 raia wa Chile atafanyiwa ukaguzi leo Juampili.
Muda wa mkataba wa Mkhitaryan na kitita atakachopokea kama mashahara hakijulikani.
Arsene Wenger awali alisema Sanchez atajiunga na United iwapo tu Mkhitaryan atahamia Arsenal.
Sanchez alikosa ushindi wa Arsenal wa mabao 4-1 dhidi ya Crystal Palace Jumamosi kwasababu alikuwa anasafiri kwenda Manchester.
"Huwezi kusafiri kwenda kaskazini na ucheze soka kwa wakati mmoja," alisema Wenger.
Mkufunzi wa United Jose Mourinho, wakatihuo huo amesema mkataba wa kumsajili Sanchez unakaribia kukamilika kufuatia ushindi wa timu yake wa bao 1-0 dhidi Burnley Jumamosi.
Timu hiyo ya Mashetani wekundu iliipiku Arsenal kumsajili Mkhitaryan kutoka Borussia Dortmund mnamo July 2016 kwa kima cha £ milioni 26.3.
Sanchez, amefunga mabao 80 katika mechi 166 za mashindano yote akiichezea Arsenal tangu kusajiliwa kutoka Barcelona mnamo July 2014 kwa £ milioni 35.
- Man City wanamtaka Alexis Sanchez
- Arsenal wakataa £50m za Alexis Sanchez
- Sanchez atarejea kuwa hatari - Wenger
Raia huyo wa Chile ambaye mkataba wake na Arsenal ulitarajiwa kumalizika msimu wa joto mwaka huu alitarajiwa kusajiliwa Manchester City mwaka jana.
Imeabinika wiki hii kwamba City iliamua kutomsajili tena.
No comments:
Post a Comment