Mshambuliaji wa Stoke na Uingereza Peter Crouch, 36, analengwa kusajiliwa na Chelsea baada ya majeruhi kumnyima Andy Carroll , 29, fursa ya kuhamia klabu hiyo.(Telegraph)
Chelsea inataka kumsajili mshambuliaji wa Bosnia Edin Dzeko, 31, na beki wa Itali Emerson Palmieri, 23, kutoka Roma. Wawili hao wanaweza kugharimu jumla ya £77m. (Daily Star)
Chelsea itamtumia mshambuliaji wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 24 kumsajili Edin Dzeko. (Sky Italia)
Kipa wa Manchester United David De Gea, 27, anasema kuwa katika klabu hiyo ni kitu maalum. Raia huyo wa Uhispania alitaka kuzima uvumi ambao umekuwa ukisambaa kuhusu hatma yake katika uwanja wa Old Trafford.(ESPN)
- Zinedine Zidane: Sioni Real Madrid bila Cristiano Ronaldo.
- Arsene Wenger adaiwa 'kuikosea heshima' Dortmund
- Neymar azomewa kwa kumnyima Cavani penalti
Manchester City wana hamu ya kiungo wa kati wa Liverpool na Ujerumani Emre Can, 24, lakini hatma yake huenda ikategemea hatua ya Liverpool ya kutaka kumsajili kiungo wa Schalke, 22 Leon Goretzka. (Mirror)
Tottenham inashindana na Manchester United katika mpango wa kutaka kupata saini ya mshambuliaji wa Paris St-Germain na Brazilian Lucas Moura, 25. (L'Equipe - in French)
Alexis Sanchez amelazimika kufanya mazeozi na timu ya vijana huku mpango wa mchezaji huyo kuelekea Old Trafford ukiendelea kuchelewa. (Times)
United wanaiongoza Liverpool na Chelsea katika harakati za kumnunua kiungo wa kati wa Nice Jean-Michael Seri, 26, huku Manchester City pia ikimtaka mchezaji huyo wa Ivory Coast. (Mirror)
Chelsea huenda ikakabiliwa na marufuku ya uhamisho kwa kukiuka sheria kuhusu usajili wa wachezaji wa kigeni walio na chini ya umri wa miaka 18. (Guardian)
Brighton inamtaka mshambuliaji wa Uholanzi na PSV Jurgen Locadia, 24. (De Telegraaf - in Dutch)
Mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 24, atalazimilka kuwasilisha ombi la uhamisho ili kupata fursa ya kujiunga na Manchester United, kulingana na afisa mkuu wa Juventus Beppe Marotta. (La Gazetta Dello Sport - in Italian)
Arsenal imepiga hatua kubwa katika kumsajili mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang baada ya mchezaji huyo ,28, kutohusishwa katika kikosi cha timu hiyo dhidi ya Hertha Berlin. (Bild - in German)
Winga wa Everton na mchezaji wa zamani wa Uingereza Aaron Lennon, 30, na mshambuliaji wa Leicester Islam Slimani, 29, wanalengwa na Newcastle ili kusajiliwa kwa mkopo. (Shields Gazette)
Besiktas pia ina hamu ya kumsajili Slimani na sasa Watford wamejiunga katika harakati za kumsajili mchezaji huyo wa Algeria (Daily Star)
Mkufunzi wa Leicester Claude Puel anasema kuwa ataamua iwapo atamnunua beki wa Austria Aleksandar Dragovic kwa mkataba wa kudumu msimu ujao. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kwa sasa yuko katika klabu hiyo kwa mkopo kutoka Bayer Leverkusen. (Leicester Mercury)
West Brom wanafanya mazungumo ya kumsaini beki wa kulia wa Basle na Switzerland Michael Lang, 28. (Mail)
Mkufunzi wa Huddersfield David Wagner amepinga kufanyika kwa uhamisho wowote licha ya klabu hiyo kuhusishwa na uhamisho wa beki wa Borussia Dortmund na Serbia Neven Subotic, 29. (Huddersfield Examiner)
Joey Barton anadai kuwa ni ''unafiki'' kwa liverpool kumfuta kazi mchezaji mwenza Jon Flanagan, 25, baada ya beki huyo wa Uingereza kupatikana na hatia ya kumpiga mpenziwe. (Talksport)
Arsenal inaelekea kuafikiana na mchezaji wa Ujerumani Mesut Ozil, 29, na kiungo wa kati Jack Wilshere, 26 kusaini kandarasi mpya. (Sun)
No comments:
Post a Comment