TANGAZO


Thursday, January 18, 2018

SIMBA YAIPIGA SINGIDA FC BAO 4-0 LIGI KUU YA VODACOM UWANJA WA TAIFA DAR ES SALAAM, OKWI ATUPIA MAWILI

Mashabiki wa timu ya Simba, wakifuatilia mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya timu hiyo, dhidi ya Singida FC, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni ambapo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 4-0, mabao mawili yakifungwa na mchezaji wao wa Kimataifa kutoka Uganda, Emmanuel Okwi, aliyeingia kipindi cha pili, akichukua nafasi ya Mghana, James Kotei.(Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mashabiki wa timu ya Simba, wakifuatilia mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya timu hiyo, dhidi ya Singida FC, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. 
Kennedy Wilson (kushoto) wa Singida FC, akiruka juu kuupiga mpira kichwa huku akiangaliwa na James Kotei (wa pili kulia) na Shiza Kichuya, aliyefunga bao la kwanza, wote wa Simba, wakati wa mchezo huo. Bao la pili la timu hiyo lilifungwa na mchezaji wao mpya, Asante Kwasi kutoka nchini Ghana.
Said Ndemla (kulia) wa Simba akipiga mpira uliompita Maliki Antiri (3), wa Singida FC.  
Maliki Antiri (3) wa Singida FC na John Bocco (22) wa Simba wakiruka juu kuwania mpira, wakati wa mchezo huo.
Emmanuel Okwi wa Simba akipiga shuti lililoipatia timu yake ya Simba bao la 3 huku akikabwa na Kennedy Wilson (kulia) wa Singida FC.
Emmanuel Okwi (kushoto), Said Ndemla (katikati) na John Bocco, wote wa Simba wakishangilia bao bao la 3 lililofungwa na Okwi katika mchezo huo. 
Emmanuel Okwi (kushoto), Said Ndemla (katikati) na John Bocco, wote wa Simba wakishangilia bao bao la 3 lililofungwa na Okwi katika mchezo huo.  
Emmanuel Okwi (katikati), Said Ndemla (kulia) na Shiza Kichuya, wote wa Simba wakishangilia bao bao la 4 lililofungwa na Okwi na kuhitimisha karamu ya mabao katika mchezo huo.  
Mashabiki wa timu ya Simba, wakishangilia bao la 4 la timu hiyo, lililofungwa na Emmanuel Okwi  katika mchezo huo, dhidi ya Singida FC, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. 
Emmanuel Okwi wa Simba akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo ambapo aliibuka shujaa kwa kuifungia timu yake mabao 2.  
Emmanuel Okwi wa Simba akizungumza na waandishi wa habari. 
Mashabiki wa timu ya Simba, wakimshangilia mchezaji wao, Emmanuel Okwi wakati akitoka uwanjani baada ya kuifungia timu yake mabao 2, Shiza Kichua 1 na Asante Kwasi 1 na hivyo timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 katika mchezo huo.

No comments:

Post a Comment