TANGAZO


Saturday, January 20, 2018

Rubani 'mlevi' atimuliwa katika ndege ya Uingereza

Rubani aliyedaiwa amelewa alilazimishwa kutoka ndege katika uwanja wa Gatwick baada ya abiria kuwa na hofu

Haki miliki ya pichaPA
Image captionRubani aliyedaiwa amelewa alilazimishwa kutoka ndege katika uwanja wa Gatwick baada ya abiria kuwa na hofu
Rubani aliyedaiwa amelewa alilazimishwa kutoka ndege katika uwanja wa Gatwick baada ya abiria kuwa na hofu.
Ndege hiyo ya Uingereza iliokuwa ikieekea Mauritius siku ya Alahamisi ilicheleweshwa kabla ya rubani huyo kutolewa na mwengine kuchukua mahala pake.
Duru za habari katika uwanja huo iliambia gazeti la The Sun: Maafisa wa polisi waliingia katika ndege hiyo kabla ya kuelekea moja kwa moja katika chumba cha rubani.
Rubani huyo alifungwa pingu na kutolewa.
Raia mmoja mwenye umri wa miaka 49 kutoka Magharibi mwa mji wa London amekamatwa na atasalia katika mikono ya maafisa hao kulingana na askari wa Sussex.
Mtu huyo kutoka eneo la Harmondsworth, magharibi mwa Drayton, amekamatwa kwa tuhuma za kutaka kuendesha ndege wakati ambapo kiwango cha pombe katika mwili wake kimezidi kiwango kilichowekwa.

No comments:

Post a Comment