Korea Kusini imeitaka Korea Kaskazini kueleza ni kwa nini imefutilia mbali mkutano ambao ungejadili tamasha za kitamaduni wakati wa michezo ya Olimpiki ya msimu wa baridi mwezi ujao.
Utawala wa Pyongyang ulikuwa umekubali kutuma wajumbe saba kuchunguza maeneo ambayo yangetumika lakini siku ya Ijumaa, utawala wa Pyongyang ukasema kuwa ziara hiyo imefutiliwa mbali.
- Korea Kaskazini kushiriki michezo ya Olimpiki
- Korea Kusini yasema iko macho kwa kaskazini
- Korea Kusini yataka mazungumzo na Korea Kaskazini kuhusu michezo
Ombi la Korea Kusini la kutaka majibu ya hatua kufikia sasa halijajibiwa na Korea Kaskazini.
Maafisa wa mataifa hayo mawili wanakutana na wanachama wa kamati kuu ya Olimpiki mjini Geneva, kujadili jinsi Korea Kaskazini inaweza kushiriki mashindano hayo ya Olimpiki.
No comments:
Post a Comment