TANGAZO


Thursday, January 18, 2018

Picha ya Selfie kwenye Facebook yasababisha muuaji kupatikana Canada

Cheyenne Antoine (L) poses with victim Brittney Gargol.

Haki miliki ya pichaFACEBOOK
Image captionMkanda unaovaliwa na Cheyenne Antoine (kushoto) unaonekana kwenye picha na rafiki yake Brittney Gargol
Mwanamme mmoja nchini Canada amepatikana na hatia ya kumuua rafiki yake baada ya polisi kugundua kuwa kifaa kilichotumiwa kuua kilichokuwa kwenye picha ya kujipiga (selfie) ya wawili hao iliyokuwa katika mtandao ya kijamiii.
Cheyenne Rose Antoine, 21, alikiri siku ya Jumatatu kumuua Brittney Gargol, 18, Machi mwaka 2015.
Gargol alipatikana amenyongwa karibu na Saskatoon, Saskatchewan, huku mkanda wa Antoine ukiwa kando na mwili wake.
Antoine alihukumiwa kifungo cha miaka saba jela kwa mauaji
Alitajwa kama mshukiwa baada ya kuchapisha picha ya selfie kwenye mtandao wa Facebook, ikionyesha amevaa mkanda uliotumika saa kadhaa kabla ya Gargol kuuliwa.
Alisema walikuwa wamekunywa pombe na pia wakavuta bangi kabla kuanza kuzozana.
Polisi wanasema kuwa taarifa ambayo alikuwa amewapa, kuwa Gargol aliondoka na mwanamume mmoja huku naye akionda kumuona shangazi yake.
Ndipo wakatumia picha zake za Facebook kufuatilia mienendo ya wawili hao usiku huo.

No comments:

Post a Comment