Korea ya Kaskazini na Korea Kusini wamekubali kuunda timu ya wanawake ya barafu ya Hockey na na kusonga katika michuano hiyo chini ya bendera moja katika michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya Korea Kusini.
Mpangilio huu unaongeza vuguvugu katika uhusiano ulioanza wakati kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un, alipotamka kuwa atatuma timu ya vijana wake kushiriki katika michuano ya mwaka huu wakati alipokuwa akitoa salamu za mwaka mpya katika hotuba yake
Kama sehemu ya msafara wake, Pyongyang itatuma wahamasiahaji michezoni wapatao mia mbili, pamoja na bendi ya ala. Makubaliano hayo yameibua matumaini mapya juu ya uwezekano wa kuwa na mazungumzo kuhusu mpango wa silaha za nyuklia za Korea Kaskazini ingawa Japan imeionya dunia kutoghilibiwa na ucheshi wenye kukera wa Korea ya Kaskazini.
No comments:
Post a Comment