Mtu mmoja amefariki nchini Tanzania baada ya kuigonga ndege iliokuwa ikipaa katika uwanja wa ndege wa Mwanza
Akizungumza kwa njia ya simu mmoja wa wafanyakazi wa kiwanja hicho cha ndege ameielezea BBC kuwa mtu huyo alivuka mpaka na kuingia eneo la uwanja wa ndege na moja kwa moja kwenye njia ya kurukia ndege ambapo alikutana na ndege ya shirika la ndege la Fast Jest iliyokuwa inaruka kuelekea jijini Dar es salaam.
Jeshi la polisi jijini Mwanza linasema tukio hilo la aina yake lilitokea usiku majira ya saa tatu Januari 17 na baada ya kuruka rubani wa ndege iliyohusika aliwajulisha wenzake kwenye mnara wa kuongozea ndege uwanjani hapo juu ya tukio hilo
- Mwanamfalme wa Saudi Arabia afariki katika ajali ya ndege
- Ndege ndefu zaidi duniani yapata ajali
- Ndege iliowabeba waandishi wa habari yaanguka Kenya
Kwa mujibu wa kaimu mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania (TAA), Richard Mayongela ambaye amethibitisha kutokea kwa tukio hilo amenukuliwa na Radio Free Afrika (RFA) akisema "Ingawa ndege ndiyo ilimgonga mtu huyo ambaye jina lake hatulifahamu, kisheria mtu au kitu chochote kinachokuwa kwenye njia ya kurukia na kutua ndege ndiyo kinahesabiwa kuigonga ndege, ni kama ilivyo kwa treni,"
Mpaka sasa haijafahamiki ilikuwaje mtu huyo akawepo kwenye njia ya kurukia ndege wakati ndege ilipokaribia kuruka licha ya ukaguzi wa njia hiyo kabla ya ndege hiyo kuruhusiwa kuanza safari yake.
Jeshi la Polisi nchini humo linaendelea na uchunguzi kubaini undani wa kisa hicho
Uwanja wa ndege wa Mwanza uko pembezoni mwa ziwa victoria na umepakana na makazi ya watu na kwa muda sasa umekuwa hauna uzio licha ya kuwa umekuwa ukitengenezwa kwa miaka kadhaa sasa
No comments:
Post a Comment