TANGAZO


Monday, January 22, 2018

Ellen Johnson Sirleaf: Utawala wa rais wa kwanza mwanamke Afrika

Ms Sirleaf mnamo 2010

Haki miliki ya pichaREUTERS
Ellen Johnson Sirleaf aliweka historia kwa kuchaguliwa kuwa rais wa kwanza mwanamke Afrika, lakini pia alikabiliwa na shutuma za rushwa na upendeleo wa kuajiri jamaa zake serikalini. Je atakumbukwaje ?
Tamthilia yake bi Sirleaf imegubikwa kwa ujasiri na ukakamavu wake uliochanganyika kwa tuhuma za rushwa na upendeleo wa kuajiri jamaa zake katika kazi za serikali.
Siku chache kabla ya kuondoka madarakani baada ya utawala wa kihistoria wa miaka 12, alitimuliwa kutoka chama chake cha kisiasa. Kuna wau wanaomtizama kama muokozi, huku wengine wanasema ni kiongozi kama viongozi wengine wote.
"Kitu bora alichotufanyia ni kutudumishia amani," amesema Jenneh Sebo mwenye umri wa miaka 22, aliyekuwa amekaa akiota jua katika mji mkuu Monrovia tulipozungumza naye Oktoba mwaka jana ukisubiriwa uchaguzi mkuu.
Hili sio jibu lisilo la kawaida. Raia wa Liberia wamekabiliwana miaka 14 ya vita vikali vilivyochochewa na vya ki unyama , ambapo watoto waliotumika kama wanajeshi walitekeleza uhalifu usiotajika. Makundi ya waasi yalitawala miji na mitaa kwa kuzusha hofu kubwa, na kuifilisi nchi hyo kimiundo mbinu.
Hospitali, shule, barabara ziliharibiwa, na hata taa za barabarani zilivunjwa kutokana na imani kuwa huedna wanajeshi hasimu wanaweza kuungana. Kwahivyo ni jambo kubwa kushukuru kuwepo amani katika taifa hilo.
Hatahivyo, miaka 15 baada ya kumalizika vita, kwa muda mrefu raia wanatarajia huduma zaidi kutoka kwa serikali. Jenneh, ambaye ni mdogo mno kukumbuka vita vilivyoshuhudiwa alikuwa amekaa juani kwasababu hana ajira na hajasoma tangu alipomaliza shule ya upili.
Mwezi huo huo, katika uwanja uliojaa nyasi kando kando mwa nyumba ya Bi Sirleaf katika mtaa wa kifahari wa Sonkor mjini Monrovia, mamia ya wanawake waliovaa nguo nyeupe waliimba na kudensi kwa muziki uliokuwa unatoka kwa sautikubwa kwenye vipaza sauti. Muimbaji alikuwa anaimba "Tunataka amani Liberia, amani Monrovia", ni wimbo ambao mwanamuziki nyota wa Ivory Coast mtindo wa reggea Alpha Blondy aliouandika kuihusu nchi yao wakati wa vita mnamo 1992.
Wanawake hawa wengi waliidhinisha kampeni ya amani mnamo 2003 iliyosaidia kumaliza vita nchini. Waliandamana hadi waume zao wakaweka silaha chini.
Wanaharakati wanawake waliosaidia kuchaguliwa kwa Bi SirleafHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWanaharakati wanawake waliosaidia kuchaguliwa kwa Bi Sirleaf
Ni wanawake hawa waliosaidia na kuishinikiza nchi kumchagua Ellen Johnson Sirleaf mnamo 2005.
Bi Sirleaf si mtu wa kujipendekeza na hakulenga masuala ya wanawake katika utawala wake wa miaka 12, Hatahivyo, mwanauchumi huyo aliyefuzu kutoka Harvard alifanikiwa deni lenya thamani ya $5bn la nchi hiyo baada ya kuhudumu kwa miaka mitatu madarakani, na kutoa nafasi kwa uwekezaji wa nje na kuongeza bajeti ya serikali kutoka $80m hadi $516m kufikia 2011.
Chini ya utawala wake, sheria mpya, na kali ya ubakaji iliidhinishwa lakini ilikarabatiwa, na kupunguza hukumu kali na kuishia kufanya hukumu ya ubakaji kuweza kuepukika kwa dhamana.
Bi Sirleaf (L) na Weah (R)Haki miliki ya pichaEPA
Image captionBi Sirleaf (Kushoto) anamkabidhi uongozi nyota wa soka ya kimataifa George Weah (kulia)
Wengi walidhani rais mwanamke atatoa nafasi kwa wanawake zaidi kuingia katika siasa. Ila na kwa mfano wa utawala wa Bi Margaret Thatcher Uingireza, kuondoka kwa Bi Sirleaf pia kunaidhinisha kuondoka kwa wanawake katika uongozi.
Kati ya wagombea 19 wa urais, kulikuwa na mgombea mmoja pekee mwanamke, Macdella Cooper, mwenye umri wa miaka 40, ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa rais anayeingia madarakani George Weah.
An Ebola victim in MonroviaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMaafisa wa afya walikuwa hawalipwi wakati janga la Ebola lilipozuka nchini
Shutuma za upendeleo zilimuandana Bi Sirleaf, kwa kuwateua wanawe watatu wa kiume katika nyadhifa kuu serikalini, hatua ambayo daima anaitetea.
Hadi jamaa zake 20 wamewahi kushikilia nyadhifa katika serikali kwa wakati mmoja. Kuhusu rushwa, mnamo mwaka 2006 alitangaza rushwa kuwa "adui mkubwa wa umma" ila aliishia kukabiliwana kashfa kadhaa.
Wafanyakazi wa serikali waliishia kutolipwa mishahara; zaidi walioathirika na kashfa hiyo ni maafisa wa afya katika kaunti ya Lofa kaskazini magharibi mwa nchi hiyo wakati janga la Ebola lilipozuka mpakani kutoka Guinea.
Virusi vya ugonjwa huo zilisababisha vifo vya watu takriban 5000, na kuathiri pakubwa nchi hiyo na mfumo wake wa afya.
Licha ya haya yote, Bi Sirleaf alikuwa mtu wa kuweka historia. Utawala wake huedna ulikabiliwa na shutuma hizo za rushwa na upendeleo, lakini ameudhihirishia ulimwengu kwamba mwanamke anaweza kuvunja uongozi uliozoeleka wa mwanamume na kukidhibiti kiti hicho.
Hilo linaonekana kuleta matumaini makubwa kwa wanawake.

No comments:

Post a Comment