Hasira inaonekana kuongezeka katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo dhidi ya rais Joseph Kabila tangu akatae kuondoka madarakani wakati muhula wake ulipomalizika Desemba 2016.
Rais Joseph Kabila, alifikia makubaliano na vyama vya upinzani kuandaa uchaguzi kabla ya mwisho wa mwaka 2017.
Na kufikia mwisho wa mwaka huo, rais Kabila alikuwa tayari ashafika kikomo cha utawala wake wa mihula miwili kikatiba.
Kuahirishwa kwa uchaguzi mkuu:
Hatua ya tume ya uchaguzi kuahirisha kwa mara nyingine uchaguzi mkuu hadi Aprili mwaka 2019 baada ya kuahirisha awali hadi mwishoni mwa mwaka jana 2017 uliongeza ghadhabu iliopo.
Corneille Nangaa, kiongozi wa tume ya uchaguzi nchini, CENI, amesema ilikuwa ni muhimu kuuharisha uchaguzi huo kutokana na kuzuka ghasia katika eneo la Kasai ya kati, hali inayotatiza usajili wa wapiga kura.
Mahakama ikatoa uamuzi baada ya hapo kwamba rais Kabila anaweza kusalia madarakani hadi pale uchaguzi mwingine utakapoandaliwa.
Tangu wakati huo, waandamanaji wamekuwa wakimiminika barabarani, na watu kadhaa wameuawa.
- Kabila: Sitowania urais tena
- Upinzani wapanga migomo na uvunjaji sheria DRC kumuondoa kabila madarakani
- Rais Kabila azuru nchini Tanzania
- Sita waliouawa katika maandamano DRC
Kanisa katoliki lenye ushawishi mkubwa nchini humo limetoa wito kwa raia kuandamana kwa amani kote nchini kushinikiza mageuzi hayo ya uongozi.
Haya ni licha ya serikali kupiga marufuku maandamano kufanyika tangu Septemba 2017 wakati maandamano ya kupinga utawala wa Kabila yalipokabiliwa na vurugu.
Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu linasema watu takriban milioni 7 wanahitaji usaidizi wa dharura wa kibinaadamu kutokana na mapigano ya kujihami nchini.
Utawala wa Kabila:
- Kabila ameshikilia madaraka tangu kuuawa kwa babake mnamo 2001.
- Kabila alishinda uchaguzi mnamo 2006 na kuwa rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
- Alifanikiwa kuiweka Congo kwenye ramani akijizatiti kuimarisha uhusiano wa kimataifa.
- Mnamo 2011 alichaguliwa kwa mara nyingine katika uchaguzi mkuu na kujinyakulia 42%.
- Aliapishwa kuiongoza Congo chini ya ulinzi mkali wa kijeshi licha ya hitilafu nyingi zilizoshuhudiwa.
Katika muda wa utawala wake, kuna hisia kuwa rais Joseph Kabila amejitenga na demokrasia na kuiweka Congo katika hali iliyokosa utulivu.
Hilo sasa linazusha hofu, hata kwa jamii ya kimataifa kuwa ongezeko la ghasia zinazoshuhudiwa kisiasa linaweza kuitumbukiza DRC katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.
No comments:
Post a Comment