TANGAZO


Monday, January 22, 2018

Cristiano Ronaldo aomba simu na kujiangalia kwenye kioo uwanjani

Cristiano Ronaldo checks his face in the front-facing camera of his attending physician's phone as he was led off the field

Haki miliki ya pichaEPA
Image captionRonaldo alikuwa amegongwa kwa kiatu kichwani
Nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo aling'aa sana uwanjani Jumapili na kufunga mabao mawili baada ya kimya cha muda.
Hata hivyo, si mabao yake mawili yaliyogonga vichwa vya habari kufuatia ushindi wao wa 7-1 dhidi ya Deportivo La Coruna.
Alipokuwa anaondoka uwanjani baada ya kuumia, aliomba simu ya rununu kutoka kwa daktari wake - kujitazama usoni, akitumia skrini ya simu kama kioo.
Watangazaji wa mechi walipokuwa wanacheza, na kusema kwamba wameona "kila kitu sasa" kutoka kwa mchezaji huyo, Ronaldo alitikisa kichwa chake, akionekana kutofurahishwa na alichokiona kwenye skrini ya simu au pia na ujumbe wa watangazaji wa mechi.
"Ronaldo amefikisha wasiwasi wake kuhusu muonekano wake kiwango kingine," Reuters waliandika baada ya mechi hiyo.
"Kisa hicho kilimuonesha Ronaldo halisi vyema zaidi, kuliko awali," tovuti nyingine ya michezo Benchwarmers iliandika.
"Ronaldo akijiangalia kwenye kioo hata akiwa uwanjani," mmoja wa waliochangia katika taarifa za BBC Sport aliandika.
Jeraha hilo lilitokana na kugongwa na mchezaji wa Deportivo La Coruna Fabian Schar kwa kiatu kichwani.
Licha ya kuchekwa na watu mtandaoni kutokana na jeraha hilo, yamkini lilikuwa mbaya kiasi kwamba iliamuliwa kwamba hangeweza kuendelea kucheza.
RonaldoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Ronaldo amekuwa makini sana kuhusu muonekano wake.
Mwaka 2011, alitangaza kwamba mashabiki wa klabu pinzani walikuwa wanamzomea kwa sababu alikuwa "tajiri, mtanashati na mchezaji stadi."
"Watu hunionea wivu," alisema. "Sina jambo jingine la kufafanua hilo."
Ushindi huo wa Real wa 7-1 ulitosha kuwavusha hadi nafasi ya nne La Liga.

No comments:

Post a Comment