TANGAZO


Wednesday, November 22, 2017

Saad Hariri aahirisha kujiuzulu kwake Lebanon

Waziri mkuu wa Lebanon Saad hariri ameamua kuahirisha kung'atuka kwake mamlakani

Image captionWaziri mkuu wa Lebanon Saad hariri ameamua kuahirisha kung'atuka kwake mamlakani
Waziri mkuu wa Lebanon Saad Hariri, amesema kuwa ameahirisha hatua ya kujiuzulu kwake kwa kipindi cha wiki mbili zijazo, ambayo alikuwa alitangaza awali akiwa nchini Saudi Arabia, siku kadhaa zilizopita.
Bwana Hariri anasema kuwa anamjibu Rais wa Lebanon, Michel Aoun.
Saad Hariri aamesema hayo baada ya kurejea mjini Beirut - hii ni baada ya ziara ya Ufaransa na Saudi Arabia ambako wiki mbili zilizopita alitangaza kujiuzulu wadhfa wa uawaziri mkuu wa nchini hiyo Lebanon.
Alidai amechukua hatua hiyo kwa sababu ametishiwa maisha na kundi la watu linaloungwa mkono na Iran.
Hatua yake hiyo iliwashtua wengi na kuingiza Lebanon katika sintofahamu kuu ya kisiasa.
Leo hii wakati huu ambao nchi hiyo inaadhimisha sikukuu ya uhuru wake, anasubiriwa ama kuifuta kauli hiyo ya kujiuzulu au kudumisha msimamo wake
Kufikia sasa rais Michel Aoun hajakubali hatua hiyo ya Hariri kujiuzulu.

No comments:

Post a Comment