TANGAZO


Monday, November 27, 2017

Nzi huwa wana bakteria wengi zaidi ya unavyodhani

House fly

Haki miliki ya pichaANA JUNQUEIRA AND STEPHAN SCHUSTER
Image captionVinywele kwenye mwili wa nzi huwavutia bakteria
Wanasayansi wamegundua kwamba nzi hubeba viini vingi vinavyosababisha magonjwa kuliko ilivyodhaniwa awali.
Nzi wa kawaida wanaopatikana nyumbani na nzi wanaopatikana sana kwenye mizoga huwa na bakteria zaidi ya aina 600, uchunguzi wa DNA umebaini.
Nzi hao huhusishwa na maradhi mengi ya binadamu ikiwa ni pamoja na magonjwa ya tumbo, sumu kwenye damu na nimonia.
Nzi hueneza bakteria kutoka eneo moja hadi jingine kwa kutumia miguu yao na madawa, utafiti umeonesha.
Katika kila hatua anayoipiga nzi, anaweza kueneza bakteria walio hai.
Mtafiti Prof Donald Bryant wa chuo kikuu cha jimbo la Penn State anasema watu walikuwa wanafahamu kwamba nzi hueneza bakteria lakini hawkauwa wanafahamu vyema ni kwa kiasi gani.

Milipuko ya magonjwa

Uchunguzi wa DNA ulitumiwa kuchunguza mkusanyiko wa bakteria waliopatikana katika nzi wa kawaida wa nyumbani (Musca domestica) na nzi wanaotegemea sana mizoga na vitu vinavyooza (Chrysomya megacephala).
Nzi wa kawaida wanaopatikana nyumbani, ambao hupatikana karibu kila eneo duniani waligunduliwa kuwa na aina 351 za bakteria.
Nzi hao wengine wenye kutegemea mizoga na vitu vilivyooza walikuwa na aina 316 za bakteria. Nzi hawa sana hupatikana katika mazingira yenye joto.
Bakteria wengi wanaweza kupatikana kwa pamoja katika nzi wote wawili.
Kichwa cha nzi anayetegemea sana mizoga na vitu vinavyoozaHaki miliki ya pichaANA JUNQUEIRA AND STEPHAN SCHUSTER
Image captionKichwa cha nzi anayetegemea sana mizoga na vitu vinavyooza
Watafiti hao wanasema mchango wa nzi katika kueneza maradhi hasa wakati wa mlipuko wa magonjwa umepuuzwa sana na mafisa wa afya.
"Hili linakufanya ufikirie sana unapoamua kununua mchanganyiko wa matunda njiani, ambayo yamekaa wazi kwa muda, ukiwa matembezini," amesema Prof Bryant.

No comments:

Post a Comment