TANGAZO


Monday, November 27, 2017

Prince Harry kumuoa mpenzi wake Meghan Markle

Meghan Markle na Prince Harry Septemba2017

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Mwanamfalme Harry atafunga ndoa na mpenzi wake Mwigizaji Mmarekani Meghan Markle, Jumba la Clarence limetangaza.
Mwanamfalme huyo, wa tano kwenye msururu wa warithi wa ufalme wa Uingereza, atafunga ndoa na Bi Markle majira yajayo ya kuchipua.
Harusi yao itafanyika katika Nottingham Cottage, Kensington Palace jijini London.
Taarifa kutoka Jumba la Clarence, linaloshughulikia masuala ya Mwanamfalme wa Wales Charles, babake Mwanamfalme Harry na William, imesema maelezo zaidi kuhusu kufanyika kwa harusi hiyo yatatolewa baadaye.
Bi Markle ni mwanawe Thomas Markle na Doria Ragland, na wawili hao wamewatakia "maisha yenye furaha".
Malkia Elizabeth na mumewe pia wamewatakia heri.
Wawili hao, ambao wamekuwa wakichumbiana tangu Julai 2016, walitangaza rasmi uchumba wao Novemba.
Taarifa imesema Mwanamfalme Harry ana furaha sana kutangaza taarifa hizo na kwamba amepokea baraka na idhini kutoka kwa wazazi wa Bi Markle.
Wawili hao walionekana hadharani mara ya kwanza Septemba mwaka huu.

No comments:

Post a Comment