TANGAZO


Sunday, November 26, 2017

IBRAHIM CLASS AWAPA WATANZANIA KILE WALICHOTARAJIA

Bondia  Mtanzania Ibrahim Class (kushoto) akipambana na Mwenzie kutoka Afrika Kusini  Koos Sibiya katika pambano la kimataifa la ngumi lenye mizunguko  kumi na mbil lililofanyika jana Jijini Dar es Salaam ambalo mtanzania huyo alishinda.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara hiyo Bw.Yusuph Singo (katikati) na Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Mohamed Kiganja wakifurahia pambano la ngumi kati ya mtanzania Ibrahim Class dhidi ya Koos Sibiya wa Afrika Kusini lililofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akimpongeza  Bondia Ibrahim Class baada ya kuibuka mshindi katika pambano la ngumi la kimataifa  lenye mizunguko kumi na mbili dhidi ya Koos Sibiya kutoka Afrika Kusini lililofanyika jana Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara hiyo Bw.Yusuph Singo. 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wananchi waliojitokeza katika pambano la ngumi la kimataifa kati ya mtanzania Ibrahim Class pamoja na Koos Sibiya kutoka Afrika Kusini lililofanyika jana Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Mohamed Kiganja.
Mabondia wanawake Felicha Mashauri (mwenye kaptula nyekundu) dhidi ya Happy Daudi wakizipiga jana Jijini Dar es Salaam wakati wa pambano la kimataifa  kati ya Ibrahim Class wa hapa nchini dhidi ya Koos Sibiya wa Afrika kusini ambapo mtanzania aliibuka kidedea.  
Bondia Haidari Mchanjo akifurahia ushindi wa mizunguko sita alioupata dhidi ya Bondia Bakari Magona  lililochezwa jana Jijini Dar es Salaam wakati wa pambano la kimataifa  kati ya Ibrahim Class wa hapa nchini dhidi ya Koos Sibiya wa Afrika kusini ambapo mtanzania aliibuka kidedea.  

Na Shamimu Nyaki-WHUSM.
MWANAMASUMBWI Ibrahim Class amewapa raha watanzania jana Jijini Dar es Salaam baada ya kumpiga Bondia Koos Sibiya kutoka Afrika Kusini katika mtanange wa kimataifa baina yao uliokuwa na mizunguko kumi na mbili.

Katika pambano hilo lililohuzuriwa na Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo  Mhe. Dkt. Harrison  Mwakyembe, Ibrahim Class alishinda katika mzunguko wa kumi na mbili ambapo ameandika historia  ya muda mrefu hapa nchini kwa mabondia kutofanya vizuri katika mashindano ya Kimataifa.

Akizungumza baada ya mchezo huo kumalizika Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amesema amefurahiswa sana na ushindi aliopata Ibrahim Class na kuahidi kumpa ushirirkiano zaidi ili aendelee kufanya vizuri katika mashindano mengine.

“Siri ya mafanikio katika Michezo ni kufanya mazoezi, kujiamini kusikiiza mafundisho ya mwalimu pamoja na nidhamu, Ibrahim Class ni mwanamasumbwi anaepaswa kuigwa na mabondia na wanamichezo wengine wote kutokana na uwezo wake wa kujituma hivyo wanamichezo wanapaswa kuiga kutoka kwake ili wafanikiwe na kuitangaza nchi yetu kimichezo.” Alisema Dkt. Mwakyembe.

Naye bondia Ibrahim Class ameishukuru Serikali kwa ushirikiano iliyompa wakati wa mazoezi mpaka leo amefanikiwa kupeperusha vyema Bendera ya Tanzania na ameahidi kuendelea kufanya vizuri zaidi kila atakapokuwa ulingoni na kushinda  mataji na mikanda mingi zaidi.

No comments:

Post a Comment