TANGAZO


Monday, December 12, 2016

SERIKALI YATOA RAI KWA WATANZANIA KUTUMIA MALIGHAFI ZA NDANI KUENDELEZA VIWANDA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru akizungumza wakati wa hafla ya kufunga maonesho ya Kwazna ya Viwanda vya Tanzania yaliyomalizika jana jijini Dar es Salaam. Takribani Viwanda vidogovidogo 362 vilishiriki katika maonesho hayo ya yaliyoanza kuanzai tarehe 07 hadi 11 Desemba 2016.(Picha zote na: Frank Shija – Maelezo)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (Viwanda) Dkt. Adelhelm Meru akipokea zawadi kutoka kwa Kikundi cha Sanaa cha Albino Revolution Cultural Troupe kwa kuthamini mchango wake katika kukuza uwekezaji kwa watuwenye ulemavu wakati wa hafla ya kufunga maonesho ya Kwanza ya Viwanda vya Tanzania jana jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (Viwanda) Dkt. Adelhelm Meru akimkabidhi Cheti cha Ushiriki wa maonesho ya Viwanda vya Tanzania mwakilishi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. James Ndege wakati wa hafla ya kufunga maonesho hayo jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendeji wa TANTRADE Bw. Edwin Rutageruka.
Baadhi ya washiriki wa maonesho ya kwanza ya viwanda vya Tanzania wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (Viwanda) Dkt. Adelhelm Meru alipokuwa akifunga maonesho hayo jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa maonesho ya kwanza ya viwanda vya Tanzania wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (Viwanda) Dkt. Adelhelm Meru alipokuwa akifunga maonesho hayo jana jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (Viwanda) Dkt. Adelhelm Meru akipokea zawadi kutoka Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya maonesho ya viwanda vya Tanzania Bibi. Neema Mhondo (kushoto) kwa kuthamini mchango wake katika kukuza viwanda nchini wakati wa hafla ya kufunga maonesho hayo jana jijini Dar es Salaam.
Na Jacquiline Mrisho - Maelezo
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa rai kwa Watanzania kutumia malighafi zinazopatikana nchini kwa ajili ya kuendeleza viwanda na kukuza uchumi wa nchi.

Rai hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (viwanda), Dkt. Adelhelm Meru alipokuwa akifunga Maonesho ya Kwanza ya Viwanda vya Tanzania yaliyoanza tangu Disemba 7 mwaka huu katika viwanja vya Sabasaba vilivyopo jijini humo.

Dkt. Meru amesema kuwa nchi ya Tanzania ina fursa kubwa ya kuendeleza viwanda na kukuza uchumi wa nchi kutokana na uwepo wa malighafi za uhakika, jiografia nzuri ya nchi kwa kuwa imepakana na nchi nyingi ambazo hazina Bandari, miundombinu bora pamoja na rasilimali watu.

“Serikali inafanya juhudi kubwa kuhakikisha viwanda vinaongezeka na kukua kufikia viwanda vya kati na vikubwa hivyo nawaomba wananchi waendelee kutumia malighafi za ndani kwani itawasaidia kupunguza gharama za uzalishaji wa bidha zao na kupelekea kila mwanachi kuweza kununua bidhaa hizo kwa bei rahisi,” alisema Dkt. Meru.

Katibu Mkuu Meru ameongeza kuwa ili kuhakikisha ajira zinaongezeka nchini na umasikini unapungua ni lazima kuwekeza zaidi katika ujasiriamali wa viwanda vidogo ambavyo ndio mwanzo na chimbuko la viwanda vikubwa.

Aidha, amewapongeza wajasiriamali kwa kutengeneza bidhaa zenye ubora na viwango vya kimataifa pia amewasihi kufanya juhudi katika kutafuta soko la nje ya nchi ili kuongeza pato la Taifa na kujenga uchumi wa nchi.

Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Edwin Rutageruka amesema kuwa kwa kiasi kikubwa malengo ya maonesho hayo yametimia kwani kwa muda wa siku 5 wajasiriamali wamepata semina mbalimbali zitakazowawezesha kuboresha biashara zao, wametangaza bidhaa zao wanazozalisha pamoja na kupata fursa kwa wazalishaji mbalimbali wa malighafi kuonana na wenye viwanda ili kuwauzia malighafi hizo.

“Ingawa malengo ya maonesho haya yametimia lakini bado kuna tatizo kwa Watanzania kutumia bidhaa zinazozalishwa hapa nchini kwetu, hivyo tunawasihi wapende bidhaa zetu kwani viwanda haviwezi kuendelea bila kuwa na soko la ndani la uhakika,” alisema.

Maonesho hayo yameandaliwa na Wizara ya Viwada, Biashara na Uwekezaji kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, yamepangwa kufanyika kila mwaka kwa nia ya kuitangaza sekta ya viwanda nchini pamoja na kutoa mafunzo mbalimbali kwa wajasiriamali juu ya kuendeleza viwanda vidogo walivyonavyo kufikia viwanda vya kati na vikubwa. 

No comments:

Post a Comment