TANGAZO


Saturday, December 3, 2016

China yalalamikia mawasiliano kati ya Trump na rais wa Taiwan

Trump alituma ujumbe kupitia Tweeter akisema amepigiwa simu na kiongozi wa Taiwan, Mama Tsai Ing-wenImage copyrightAP
Image captionTrump alituma ujumbe kupitia Tweeter akisema amepigiwa simu na kiongozi wa Taiwan, Mama Tsai Ing-wen
Wizara ya mashauri ya nchi za nje ya Uchina, inasema kuwa imepeleka malalamiko kwa upande unaohusika wa Marekani, baada ya Rais mteule Donald Trump, kuzungumza kwa simu na rais wa Taiwan.
Uchina inaona Taiwan kuwa ni jimbo lake lilojitenga.
Msemaji wa wizara alisema, Uchina ni moja, na ndio msingi wa kisiasa katika uhusiano baina ya Marekani na Uchina.
Mazungumzo ya simu baina ya Bwana Trump na Rais wa Taiwan, Tsai Ing-wen, yamevunja msimamo wa kidiplomasia kwa Marekani.
Ofisi ya rais wa Taiwan ilitoa picha ikionyesha Rais Tsai Ing-we akiongea kwa simu na TrumpImage copyrightREUTERS
Image captionOfisi ya rais wa Taiwan ilitoa picha ikionyesha Rais Tsai Ing-we akiongea kwa simu na Trump
Hapo awali, waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uchina, Wang Yi, alisema mazungumzo hayo ya simu ni "ujanja wa Taiwan usiokuwa na maana".
Mwandishi wa BBC anasema ikiwa simu hiyo ni ishara ya mabadiliko ya sera za Marekani kuhusu Taiwan, basi Uchina itajibu kwa hasira.

No comments:

Post a Comment