TANGAZO


Saturday, December 3, 2016

Santos kujiuzulu kabla ya uchaguzi wa mwaka ujao

Dos Santos, ambaye ana umri wa miaka 74 alishinda uchaguzi wa kuwa Rais akiwa na umri wa miaka 34 pekee.Image copyrightAFP
Image captionDos Santos, ambaye ana umri wa miaka 74 alishinda uchaguzi wa kuwa Rais akiwa na umri wa miaka 34 pekee.
Kituo cha radio cha Angola kinasema kwamba, Rais Jose Eduardo dos Santos, ambaye ametawala taifa hilo kwa karibu miongo minne atajiuzulu kabla ya Uchaguzi, mwaka ujao.
Waziri wa Ulinzi, Joao Lourenco, anatarajiwa kuwa mkuu wa chama kinachotawala cha MPLA.
Hii ni kumaanisha kuwa yeye atakuwa Rais iwapo chama chake kinashinda uchaguzi mwaka ujao.
Bwana Dos Santos, ambaye ana umri wa miaka 74, wakati mmoja alikuwa kiongozi mchanga zaidi katika Bara la Afrika aliposhinda uchaguzi wa kuwa Rais akiwa na umri wa miaka 34 pekee.
Amewahi kusema kuwa hatashiriki uchaguzi lakini baadaye akabadilisha maoni yake na kusimama tena.
Makundi ya kupambana na ufisadi yamemlaumu kwa kuendesha serikali kama biashara ya kibinafsi.

No comments:

Post a Comment