Majirani wa Sudan Kusini pamoja na mataifa kadhaa ya magharibi yameshutumu wito wa kiongozi wa waasi nchini humo wa kutaka kuanza kwa vita vipya.
Mwezi uliopita, aliyekuwa makamu wa rais nchini humo Riek Machar alitaka makundi yanayomuunga mkono kuanzisha vita dhidi ya serikali ya Salva Kiir
Bwana Machar alilazimika kutoroka mji mkuu wa Juba ,na sasa yuko mafichoni.
Taarifa ya pamoja ya Igad,EU,Marekani,Uingereza na Norway ilionyesha wasiwasi kuhusu vita nchini humo katika majuma ya hivi karibuni.
Taarifa hiyo imelaumu serikali na makundi ya wapiganaji.
No comments:
Post a Comment