*Wapongeza siku za kuhifadhi mizigo
kuongezwa
*Wasifu kupungua kwa vituo vya ukaguzi
Baadhi ya waandishi wa habari wakimfuatilia kwa makini
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Congo (DRC) nchini Tanzania Bw. Sumail Edward
(mwenye suti) wakati alipokuwa akielezea kuridhika na uamuzi wa Serikali ya
Tanzania kuondoa vikwazo katika Bandari ya Dar es Salaam na kupelekea
wafanyabiashara wa Congo (DRC) kuendelea kuitumia bandari hiyo.
Na Frank Shija,
Maelezo
WAFANYABIASHARA
kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wafurahishwa na hatua zilizochukuliwa
na Serikali ya Tanzania katika kuondoa vikwazo vya usafirishaji wa mizigo
kupitia Bandari ya Dar es Salaam.
Hayo yamebainishwa na
Rais wa Wafanyabiashara wa Congo waishio nchini Tanzania Bw. Sumaili K. Edward
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kurejea kwao na kutumia
Bandari hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Sumaili amesema kuwa
miaka ya nyuma kulikuwa na changamoto nyingi ambapo alizitaja kuwa ni mizani na
sehemu za ukaguzi kuwa nyingi pamoja na siku za kuhifadhi mizigo kuwa chache.
Alisema kuwa
wamefikia uamuzi wa kuendelea kutumia Bandari ya Dar es Salaam baada ya
Serikali ya Awamu ya Tano kutatua changamo hizo ambapo sasa vizuizi vimepungua.
“Naipongeza Serikali
ya Tanzania kwa hatua ya kutuondolea usumbufu sisi wafanyabiashara wa Congo
tuliokuwa tunafanya shughuli zao Bandari ya Dar es Salaam, tumerejea na
tutapitishia mizigo yetu hapa”. Alisema Sumaili.
Adhai alisema kuwa
wamefarijika kuona sasa siku za kuhifadhi mizigo kabla ya kuongezeka kutoka siku 15 zilizokuwepo awali hadi kufikia 30
kama ilivyobainishwa wakati wa ziara ya siku tatu ya Rais wa Jamhuri wa
Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila mapema wiki hii.
Akijibu swali la la mwandishi
wa habari aliyetaka kujua sababu zilizowafanya kusitisha kwa muda kutumia
Bandari ya Dar es Salaam, Rais huyo alisema kuwa kitu kikubwa kilicho wafanya
wachukue uamuzi wa kusitisha ni gharama kuwa kubwa hivyo kupelekea kufanya
biashara isiyokuwa na faida.
No comments:
Post a Comment