TANGAZO


Wednesday, October 5, 2016

SERIKALI KUIJENGA SHULE YA MSINGI ILEEGA NA KUIKABARABTI SHULE YA NYAMILIMA

Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Eng. Stella Manyanya (kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Kanali Mstaafu Shaban Lissu wakati alipowasili katika Shule ya Msingi ya Nyamilima kukagua athari za tetemeko la ardhi katika shule hiyo 4/10/2016 Mkoani Kagera.
Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Eng. Stella Manyanya (aliyetangulia mbele) akiingia ndani ya moja ya madarasa katika Shule ya Msingi ya Nyamilima kukagua athari za tetemeko la ardhi katika shule hiyo 4/10/2016 Mkoani Kagera.
Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Eng. Stella Manyanya akimsikiliza mwanafunzi jinsi ya kusoma ndani ya moja ya madarasa katika Shule ya Msingi ya Nyamilima wakati wa kukagua athari za tetemeko la ardhi katika shule hiyo 4/10/2016 Mkoani Kagera.
Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Eng. Stella Manyanya akiongea na wanafunzi wa Shule ya Msingi Nyamilima ndani ya moja ya madarasa katika shule hiyo wakati wa kukagua athari za tetemeko la ardhi katika shule hiyo 4/10/2016 Mkoani Kagera.
Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Eng. Stella Manyanya (wa pili kulia) akimsikiliza Mkuu wa Shule ya Msingi Nyamilima Bw. Josam John (wa pili kushoto) wakati alipowasili katika Shule ya Msingi ya Nyamilima kukagua athari za tetemeko la ardhi katika shule hiyo 4/10/2016 Mkoani Kagera.
Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Eng. Stella Manyanya (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Shule ya Msingi Nyamilima Bw. Josam John (kushoto) wakati akijibu swali la kwanini baadhi ya walimu wa shule hiyo hawaonekani shuleni mara alipowasili katika Shule ya Msingi ya Nyamilima kukagua athari za tetemeko la ardhi katika shule hiyo 4/10/2016 Mkoani Kagera.
Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Eng. Stella Manyanya (katikati) akimuonya Mkuu wa Shule ya Msingi Nyamilima Bw. Josam John (wa pili kulia) kuhusu utoaji ruhusa ovyo kwa walimu wakati wa saa za kazi shuleni hapo mara alipowasili katika Shule ya Msingi ya Nyamilima kukagua athari za tetemeko la ardhi katika shule hiyo 4/10/2016 Mkoani Kagera.
Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Eng. Stella Manyanya akiwafurahia wanafunzi wa Shule ya Msingi Nyamilima ndani ya moja ya madarasa katika shule hiyo kwa kuweza kujibu moja ya swali alilowauliza wakati wa kukagua athari za tetemeko la ardhi katika shule hiyo 4/10/2016 Mkoani Kagera.
Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Eng. Stella Manyanya (kulia) akimpa zawadi ya fedha mmoja wa wanafunzi ambaye alijibu swali kikamilifu ndani ya darasa la Shule ya Msingi Nyamilima wakati wa kukagua athari za tetemeko la ardhi katika shule hiyo, 4/10/2016 Mkoani Kagera.
Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Eng. Stella Manyanya (kushoto) akimshauri jambo Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Kanali Mstaafu Shaban Lissu wakati (kulia) baada ya kutembelea shule ya Msingi Nyamilima kukagua athari za tetemeko la ardhi katika shule hiyo 4/10/2016 Mkoani Kagera.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Eng. Stella Manyanya (kulia) akimpa mkono wa pole Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ileega iliyopo Wilayani Kyerwa mkoani Kagera baada ya Shule yake kukumbwa na tetemeko la ardhi na kuathiri baadhi ya vyumba vya madarasa pamoja na nyumba ya Walimu hivi karibuni.

Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Eng. Stella Manyanya (aliyetangulia mbele) akiingia ndani ya moja ya madarasa lililokumbwa na tetemeko la ardhi Wilayani Kyerwa mkoani Kagera kujionea athari za tetemeko hilo katika shule ya Msingi Ileega 4/10/2016.

Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Eng. Stella Manyanya pamoja na Viongozi wa Serikali na Walimu wa Shule ya Msingi Ileega wakiangalia nyumba ya Walimu iliyoathiriwa na tetemeko la ardhi kipindi cha hivi karibuni Wilayani Kyerwa Mkoani Kagera.
Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Eng. Stella Manyanya akiongea na wanafunzi wa darasa la tatu wa Shule ya Msingi Ileega wakati wa kukagua athari za tetemeko la ardhi katika shule hiyo 4/10/2016 Mkoani Kagera.
Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Eng. Stella Manyanya (kulia) akiwaelekeza jambo Viongozi wa Wilaya ya Kyerwa baada ya kutembelea shule ya Msingi Ileega kukagua athari za tetemeko la ardhi katika shule hiyo 4/10/2016 Mkoani Kagera.
Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Eng. Stella Manyanya akiongea na wakazi wa Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera mara baada ya kukamilisha ukaguzi wa atahri za tetemeko katika shule za Nyamilima na Ileega zilizopo wilayani hapo 4/10/2016 Mkoani Kagera.

Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Eng. Stella Manyanya (wa nne waliosimama) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa eneo hilo pamoja na watendaji wa Wizara yake katika eneo maarufu la hija lijulikanalo kama Nyakijoga lililopo Wilayani Missenyi Mkoani Kagera.(Picha/Habari na Benedict Liwenga-WHUSM)
SERIKALI imepanga kuijenga shule ya msingi ileega na kufanya ukarabati wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya msingi Nyamilima zote zilizopo wilayani kyerwa mkoani Kagera kufuatia uharibifu uliotokana na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani huko mapema mwezi Septemba mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya alipofanya ziara wilayani huko kuangalia athari za tetemeko katika sekta na elimu.

Mhe. Manyanya alisema kuwa kama Serikali imejikita katika kurudisha miundombinu ya umma ikiwemo shule ili kuwawezesha wanafunzi kuendelea na masomo kama kawaida, hivyo ameitaka jamii kushirikiana na Serikali katika kurudisha miundombinu hiyo kwa maendeleo yao wenyewe na watoto wao.

“Tumeona hali ni mbaya kwenye shule hizi mbili na sisi kama serikali hatuwezi kuliacha suala hili lazima tuzikarabati na kuzijenga zile zinazohitaji kujengwa upya na dhumuni ni kuhakikisha wanafunzi wanaendelea na masomo na kuondokana na changamoto hii: Alisema Mhandisi Manyanya
Aidha Mhandisi Manyanya amemtaka mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Nyamilima kuacha tabia ya kutoa ruhusa hovyo kwa walimu suala ambalo linaathiri taaluma kwa wanafunzi.

Amewataka baadhi ya Walimu wenye tabia ya utoro wakati wa saa za kazi kuacha tabia hiyo mara moja kwani watakaobainika watachukuliwa hatua ikiwemo kufukuzwa kazi.

Wakati huohuo Mhandisi Manyanya amesema walimu watakaoshindwa kuwawezesha wanafunzi wao kujua kusoma na kuandika watashushwa vyeo vyao pasipo kumuonea mtu.

No comments:

Post a Comment