TANGAZO


Wednesday, October 5, 2016

MKUTANO BAINA YA MJUMBE WA WAZIRI MKUU WA UINGEREZA NA WIZARA YA NISHATI NA MADINI

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe (kulia) akizungumza wakati wa mkutano wa kujadili fursa za uwekezaji kwenye Sekta ya Nishati nchini hususan nishati jadidifu. Katikati ni Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza, anayeshughulikia Biashara na Uwekezaji kwa Tanzania, Lord Hollick.Kushoto ni Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Cooke. 
Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke (kushoto) akizungumza wakati wa mkutano huo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James na katikati ni Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza, anayeshughulikia Biashara na Uwekezaji nchini, Lord Hollick. 
Wajumbe kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake wakifuatilia majadiliano ya fursa za uwekezaji na Ujumbe kutoka Serikali ya Uingereza. Kushoto ni Kamishna Msaidizi anayeshughulikia Umeme, Mhandisi Innocent Luoga akifuatiwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji- Uwekezaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Declan Mhaiki. 
Wajumbe wa mkutano uliokuwa ukijadili fursa za uwekezaji katika Sekta ya Nishati nchini wakiendelea na mkutano husika ulioongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe (katikati mbele). Upande wa kushoto ni Ujumbe kutoka Serikali ya Uingereza na kulia ni Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Tanesco na REA. 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe (kulia) akimsikiliza Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza, anayeshughulikia Biashara na Uwekezaji kwa Tanzania, Lord Hollick. 
Ujumbe kutoka Serikali ya Uingereza ukiongozwa na Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza, anayeshughulikia Biashara na Uwekezaji nchini, Lord Hollick (kulia) aliyeambatana na Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke (wa pili kulia) wakijadiliana jambo.

Na Mohamed Seif, Nishati na Madini
MJUMBE wa Waziri Mkuu wa Uingereza, anayeshughulikia Biashara na Uwekezaji kwa Tanzania, Lord Hollick ametembelea Wizara ya Nishati na Madini na kufanya mazungumzo na Naibu Katibu Mkuu, Profesa James Mdoe kuhusiana na masuala ya uwekezaji kwenye Sekta ya Nishati nchini.

Hollick na ujumbe wake ambao uliongozana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Cooke walieleza nia ya kampuni za nchini  Uingereza kuwekeza nchini hususan kwenye uzalishaji umeme kwa kutumia nishati jadidifu.

Alisema kampuni za Uingereza zipo tayari kuwekeza nchini na kuwa zinayo teknolojia ya kisasa kwa ajili ya uwekezaji wa aina hiyo hususan ikizingatiwa kuwa Tanzania fursa za uwekezaji wa kutumia nishati jadidifu zipo nyingi na alipendekeza wataalamu wa Wizara pamoja na Taasisi zake ziandae mada zinazoonyesha maeneo yanayohitaji uwekezaji wa aina hiyo.

Akizungumza wakati wa Mkutano huo, Profesa Mdoe alisema fursa za uwekezaji ni nyingi na alizikaribisha kampuni zote zenye nia ya kuwekeza nchini zifanye hivyo bila kusita na kwamba Wizara ya Nishati na Madini kwa kushirikiana na Taasisi zilizo chini yake zikiwemo Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania itatoa ushirikiano wa kutosha ili kuwepo na uwekezaji wenye tija kwa kampuni husika na kwa Taifa.

No comments:

Post a Comment