TANGAZO


Tuesday, October 4, 2016

MAKAMU WA RAIS WA CUBA ATEMBELEA KIWANDA CHA KUZALISHA VIUADUDU WA KUUA VILUWILUWI VYA MBU WANAOAMBUKIZA MALARIA MKOANI PWANI

Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Salvador Valdes Mesa (kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Bw. Mlingi Mkucha wakati makamu uyo alipofanya ziara katika kiwanda cha kuzalisha viuadudu wa kuua viluwiluwi wa mbu wanaoambukiza malaria mkoani Pwani. Kushoto kwa makamu wa Rais wa Cuba ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee  na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu. 
Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Salvador Valdes Mesa (kushoto), akisalimiana na Meneja wa Kiwanda cha Biotec Product ambacho kinazalisha viuadudu wa kuua viluwiluwi wa mbu wanaoambukiza malaria, Bw. Alejandro Torres, kilichopo Mkoani Pwani. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), Dkt Samuel Nyantahe akizungumza jambo wakati akimkaribisha Makamu wa Rais wa Cuba Mhe. Salvador Valdes Mesa katika kiwanda cha kuzalisha viuadudu wa kuua viluwiluwi wa mbu wanaoambukiza malaria mkoani Pwani. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Mlingi Mkucha akizungumza jambo mbele ya Makamu wa Rais wa Cuba Mhe.Salvador Valdes Mesa wakati makamu uyo alipotembelea kiwanda cha kuzalisha viuadudu wa kuua viluwiluwi wa mbu wanaoambukiza malaria mkoani Pwani. Katikati ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee  na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu. 
Makamu wa Rais wa Cuba Mhe. Salvador Valdes Mesa akisisitiza jambo wakati alipotembelea kiwanda cha kuzalisha viuadudu wa kuua viluwiluwi wa mbu wanaoambukiza malaria mkoani Pwani.Kulia kwake ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee  na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Mlingi Mkucha  na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo. 
Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Salvador Valdes Mesa (kushoto) na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee  na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (katikati), wakimskiliza Meneja Teknolojia wa kiwanda cha Biotec Product, Bi. Lourdes Gonzalez (kulia), kinachozalisha viuadudu wa kuua viluwiluwi wa mbu wanaoambukiza malaria mkoani Pwani.(Picha zote na Daudi Manongi, Maelezo)

No comments:

Post a Comment