TANGAZO


Tuesday, October 4, 2016

DRC KUENDELEA KUTUMIA ZAIDI BANDARI YA DAR ES SALAAM

Rais Joseph Kabila
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Joseph Kabila akipokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli wakati alipowasili katika jengo la Mamlaka ya Bandari ya Tanzania kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi mapema hii leo jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Eliphace Marwa – Maelezo)
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Joseph Kabila kushoto pamoja na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli wakitoa heshima kwa wimbo wa Taifa wakati wa sherehe za kuwekaji jiwe la msingi katika Jengo la Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) mapema hii leo jijini Dar es Salaam ambapo Rais wa Kabila alikuwa mgeni rasmi. 
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania Bw. Deusdedit Kakoko akitoa neno la utangulizi kwa Marais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Joseph Kabila na wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli (hawapo pichani) wakati wa sherehe za kuwekaji jiwe la msingi katika Jengo la Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) mapema hii leo jijini Dar es Salaam ambapo Rais wa Kabila alikuwa mgeni rasmi. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akielezea historia fupi ya mradi “One Stop Centre” ulio chini ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kabla ya sherehe za uwekaji jiwe la msingi uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Joseph Kabila mapema hii leo jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akisisitiza jambo kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria sherehe za kuwekaji jiwe la msingi katika Jengo la Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) mapema hii leo jijini Dar es Salaam ambapo Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Joseph Kabila alikuwa mgeni rasmi. 
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Wakandarasi wa Jengo la Mamlaka hiyo wakimskiliza kwa makini Mgeni Rasmi Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Joseph Kabila wakati alipokuwa akielezea nia ya nchi yake kuitumia bandari ya Dar es Salaam mapema hii leo wakati wa uzinduzi wa jengo la kitega uchumi la mamlaka hiyo “One Stop Centre” mapema hii leo jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Joseph Kabila akielezea dhamira ya nchi yake kuitumia bandari ya Dar es Salaam kwa wafanyakazi wa mamlaka hiyo (hawapo pichani) wakati wa sherehe za kuwekaji jiwe la msingi katika Jengo la Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) mapema hii leo jijini Dar es Salaam ambapo Rais wa Kabila alikuwa mgeni rasmi. 
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Joseph Kabila akifunua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa jiwe la msingi katika jengo la kitega uchumi la Mamlaka ya Bandari Tanzania “One Stop Centre” mapema hii leo jijini Dar es Salaam ambapo Rais wa Kabila alikuwa mgeni rasmi. 
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Joseph Kabila na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi pamoja na Mawaziri toka Kongo (DRC) na Tanzania. 

Na Immaculate Makilika- Maelezo
RAIS wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila, amesema Serikali yake  itaendelea kutumia bandari ya Dar es Salaam kupitishia mizigo yake ili kuendeleza ushirikiano na  manufaa ya kiuchumi baina ya wananchi wa nchi hizo.

Akizungumza  na waandsihi wa habari leo Ikulu jijini  Dar es Salaam mara baada ya kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Magufuli, alisema kuwa nchi ya Kongo imekua ikitumia  Bandari ya  Dar es Salaam  tangu hapo awali, na sasa wanatarajia kutumia bandari hiyo kwa kupitisha mizigo zaidi.

“Tunatarajia kufanya biashara zaidi na Bandari ya Dar er salaam kwa kupitisha mizigo kwa wingi, miaka ya nyuma tulikua na matataizo kidogo ila kwa sasa kuna kazi kubwa inafanyika ya kuboresha Bandari ya Dar es salaam na sisi tutaweza kupitisha mizigo yetu kwa wingi” alisema Rais Kabila.

Aidha Rais Kabila alisema kuwa katika mazungumzo yake na Rais Magufuli walijadili masuala mbalimbali ikiwemo hali ya usalama katika mipaka ya Kongo na uwekezaji.

Kwa upande wake Rais Magufuli, alisema kuwa  katika kuboresha usafirishaji mizigo kwenda nchini Kongo,   Bandari ya Dar es salaam imepunguza maeneo ya vituo vya kupima mizigo ambapo kwa sasa kuna maeneo matatu yenye vituo vya kupimia mizigo ambavyo ni Vigawanza, Manyoni na Nyakaliwa.

Ambapo pia Bandari hiyo imeongeza kipindi cha msamaha wa kuhifadhi mizigo bandarini kutoka nchini  Kongo kutoka  siku 14 hadi siku 30.

Aidha, Rais Magufuli alisema kuwa biashara kati ya Tanzania na Kongo imendelea kuimarika  hadi kufikia shilingi  bilioni Tsh. 393.6 kutoka Tsh. Bilioni 23.1 kwa mwaka 2009.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Sospeter Muhongo na Waziri wa Mafuta wa Kongo  Mhe. Ngoyi Makena wametia saini mkataba wa makubaliano wa kutafuta mafuta katika ziwa Tanganyika.

Ziara ya Rais wa Kongo nchini  inalenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia pamoja na kukuza maendeleo ya uchumi baina ya  nchi hizo mbili.

No comments:

Post a Comment