TANGAZO


Saturday, October 8, 2016

Madhehebu ya Shia yapigwa marufuku katika jimbo la Nigeria

Mamia ya waumini wa madhehebu ya Shia waliandamana NIgeria kupinga msako wa jeshi mwaka jana

Image copyrightAHMED MUSA
Image captionMamia ya waumini wa madhehebu ya Shia waliandamana NIgeria kupinga msako wa jeshi mwaka jana
Maafisa katika jimbo la Kaduna Nigeria wameharamisha vuguvugu la kiislamu Nigeria - Islamic Movement of Nigeria - kundi kuu la madhehebu ya shia nchini humo.
Kwa kunukuu sheria kadhaa - serikali ya jimbo hilo imesema uamuzi wa kulipiga marufuku kundi hilo ni katika kuhakikisha amani na usalama katika jimbo hilo la kaskazini magharibi.
Serikali inasema tangu kuzuka ghasia kat iya jeshi na kundi hilo la kiislamu mnamo Desemba mwaka jaba - wafuasi wa kundi hilo wameendelea kuvunja sheria.
Jambo ambalo maafisa wa serikali katika eneo hilo wanasema hawawezi kulipuuza.
Kwa amri hii, msemamji wa serikali hiyo ameongeza kuwa kuanzia sasa mtu yoyote anayejihusisha au akatekeleza mambo kwa jina la kundi hilo atashtakiwa.
Waumini wa Shia NigeriaImage copyrightAFP
Image captionWaumini wa Shia Nigeria
Makao makuu a kundi hilo ni mji wa Zaria kaskaizni magharibi mwa jimbo la Kaduna.
Inaslia kuonekana ni vipi amri hii itaathiri matawi mengine ya kundi hilo nchini.
Tume ya mahakama ilipendekeza kushatakiwa wote waliohusika katika mapigano kati ya jeshi na madhehebu ya Shia ambapo jeshi lilituhumiwa kwa kuawaia wafuasi 347 wa kundi hilo.
Mpaka sasa hakuna aliyeshtakiwa.
Mwanajeshi mmoja pia aliauwa katika ghasia hizo.

No comments:

Post a Comment