TANGAZO


Thursday, July 28, 2016

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AYATAKA MABARAZA YA MADIWANI KUFANYA MAPITIO YA UPUNGUFU WA VYUMBA VYA MADARASA KATIKA HALMASHAURI NCHINI

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa  pamoja na Balozi wa Kuwait Mhe Jaseem Al Najem  wakiwa wamekaa katika  madawati ambayo yametolewa na Ubalozi wa Kuwait wakati wa hafla ya makabidhiano ya madawati 300 ikiwa ni sehemu ya madawati 600 ambayo ubalozi huo umeahidi kutoa kwa Serikali mapema hii leo katika shule ya Msingi Chamanzi iliyopo wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Eliphace Marwa -Maelezo)
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa  akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mabohora nchini Bw.Zainudin Adamje wakati wa hafla yaMakabidhiano ya madawati 105 kati ya 250 ambayo Jumuiya hiyo imeahidi kutoa kwa serikali mapema hii leo katika shule ya Msingi Chamanzi iliyopo wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi  Dkt. Augustine Mahiga. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) akimkabidhi  hundi Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa hafla ya makabidhiano  madawati  ikiwa ni fedha zilizochangwa na watumishi wa wizara hiyo ikiwa sehemu ya kutekeleza agizo la Rais Mhe. John Magufuli  mapema hii leo katika shule ya Msingi Chamanzi iliyopo wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam. 
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa  akimkabidhi hundi Msimamizi wa kikosi Kazi cha Utengenezaji Madawati Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Magereza John Masunga wakati wa hafla ya makabidhiano  madawati  mapema hii leo katika shule ya Msingi Chamanzi iliyopo wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam . 
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa  akifurahia jambo wakati akiongea katika hafla ya makabidhiano madawati ilyofanyika mapema hii leo katika shule ya Msingi Chamanzi  iliyopo wilaya ya Temeke jijini dare s Salaam, kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Mwenyekiti wa  Jumuiya ya Mabohora nchini Bw. Zainudin Adamje  na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi  Dkt. Augustine Mahiga.

Na Beatrice Lyimo, Maelezo, Dar es Salaam
2016-07-28
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa ametoa maagizo kwa Mabaraza ya Madiwani nchini kufanya mapitio katika shule zote za Halmashauri ili kujua upungufu wa madarasa na kuanza mkakati wa utekelezaji wa  ujenzi wake.

Aliyasema hayo leo, wakati akipokea mchango wa madawati kwa shule ya msingi Chamazi kutoka Wizara Ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais la upatikanaji wa madawati katika shule za msingi na sekondari nchini. 

Mhe. Majaliwa alisema  suala la upatikanaji wa madawati linakwenda sambamba na ujenzi wa madarasa hivyo ni wajibu wa kila halmashauri kuweka mkakati wa ujenzi wa vyumba vya madarasa kwani elimu bora ni pamoja na kuwa na mazingira rafiki ya kusomea.

‘Mbali na utekelezaji wa agizo la Rais juu ya mkakati wa upatikanaji wa madawati, suala hili linakwenda sambamba na ujenzi wa madarasa hivyo Serikali imeanza utekelezaji wa ujenzi huo  kwa maeneo machache hivyo ni jukumu la halmashauri kuhakikisha mnaandaa mikakati ya kuongeza vyumba vya madarasa’ alisema Majaliwa.

Aidha Waziri Mkuu Majaliwa alisema kuwa Serikali imeanza mkakati wa utekelezaji wa mpango wa  kutumia mfumo mpya wa upandishaji  madaraja walimu kwa kuwa  mfumo wa uliuotumika awali haukuwa na tija kwa maslahi ya walimu nchini.

Akipokea madawati hayo Waziri mkuu alisema kuwa anajua shida iliyopo ya upungufu wa madawati katika wilaya ya Temeke hivyo na kugawa madawati hayo katika shule tatu zilizopo katika Wilaya hiyo ikiwemo shule ya msingi Chamazi, shule ya msingi Mbande pamoja na shule ya msingi Majimatitu .

Kwa upande wake Waziri wa Wizara Ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi  Augustine Mahiga alisema  wizara yake ina jukumu la kuhakikisha inaitangaza nchi ili kuvutia wawekezaji na kukuza uchumi wa nchi, na kuongeza kuwa elimu bora ni msingi imara katika kufanikisha hilo.

Waziri Mahiga alisema Ubalozi wa Kuwait nchini pamoja na Jumuiya ya Mabohora wameikabidhi Serikali jumla 405 ili kuunga mkono jitihada za Rais ikiwemo
“Serikali ya Kuwait kupitia Ubalozi wake hapa nchini wametoa madawati  300 na kuahidi kutoa mengine 300 na Jumuiya ya Mabohora nao wamechangia madawati 105” alisema Balozi Mahiga.

Kwa mujibu wa Waziri Mahiga alisema watumishi wa Wizara yake walichanga kiasi cha Tsh. Milioni 100 ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha umma ili kuhamasisha umma kuhusu zoezi la upatikanaji wa madawati katika shule za msingi na Sekondari nchini.

No comments:

Post a Comment