TANGAZO


Thursday, July 28, 2016

WAZIRI PROFSEA MBARAWA AMTEUA ELIUD NYAUHENGA KUWA KAIMU MENEJA BODI YA MFUKO WA BARABARA (RFB)

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profsa Makame Mbarawa

Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amemteua Bw. Eliud Nyauhenga kuwa Kaimu Meneja wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB).

Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri huyo iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam inaeleza kuwa, uteuzi huo umefanyika baada ya Meneja wa Bodi hiyo Bw. Joseph Haule kumaliza mkataba wake.

“Kwa mamlaka niliyonayo chini ya Sheria ya Bodi ya Mfuko wa Barabara Sura 220 ya mwaka 2006, nimemteua Bw. Eliud Nyauhenga kuwa Kaimu Meneja wa Bodi ya Mfuko wa Barabara tangu Julai 27 mwaka huu”, alisema Mbarawa.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa, kabla ya uteuzi huo  Bw. Eliud Nyauhenga alikuwa Meneja Msaidizi wa Bodi hiyo.

Aidha, katika taarifa hiyo, Waziri huyo amempongeza Bw. Joseph Haule kwa kuuongoza Mfuko huo kwa weledi, uadilifu na mafanikio makubwa tangu ulivyoanzishwa mwaka 2000.

Bodi ya Mfuko wa Barabara ilianzishwa kwa Sheria Na. 11 ya mwaka 1998 chini ya Sheria ya Ushuru wa Barabara Na.2 ikiwa na jukumu la kusimamia makusanyo, matumizi na ufuatiliaji wa Bodi hiyo.

No comments:

Post a Comment