TANGAZO


Thursday, July 28, 2016

HOTUBA YA RAIS WA SIMBA SPORTS CLUB EVANS AVEVA WAKATI WA KUZINDUA WIKI YA SIMBA NA SIMBA DAY 2016

Mwakilishi wa Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya EAG Group, Richard Ryaganda, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Simba, jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva.(Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva (kulia) na Mwakilishi wa Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya EAG Group, Richard Ryaganda, wakionesha kipeperushi cha Simba ikiwa ni uzinduzi rasmi wa Simba Daya na Wiki ya Simba, jijini Dar es Salaam leo.  

Viongozi wenzangu wa Simba,
Mwakilishi wa Afisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group, Richard Ryaganda,
Waandishi wa habari,
Mabibi na mabwana,

Habari za asubuhi,
Napenda niwashukuru sana kwa kufika kwenu hapa, pia kwa namna ya kipekee niwashukuru kwa kuendelea kuwapa habari Watanzania kupitia vyombo vyenu.

Kama wengi mnavyojua kila mwezi Agosti, Simba inasherehekea wiki maalum iliyobatizwa jina la Simba Week ambayo hufikia kilele chake tarehe 8 Mwezi wa Agosti. 

Mwaka huu siku hii itakuwa na uzito wa kipekee kwani Klabu ya Simba itakuwa inaanza sherehe za kuadhimisha miaka 80 ya klabu yetu tukufu.

Sherehe za Wiki ya Simba zinaenda sambamba na dhima yetu ya kuendeleza mabadiliko chanya ndani ya Simba bado inaendelea kushika kasi, Katika kipindi cha mwaka mzima, mmekuwa mashuhuda wa Simba inayolenga kuleta mapinduzi makubwa katika jinsi mpira unavyoendeshwa, kujali wanachama, utoaji wataarifa kwa wapenzi na wanachama wake na kukuza vyanzo vya mapato na kuangalia njia zenye kuweza kuongeza ufanisi na maendeleo ya timu yetu ya Simba.

Ndugu wanahabari,
Kama nilivyoeleza awali, Simba imekuwa na utaratibu wa kuwa na siku maalum kwa ajili ya kufurahi, kuwatambulisha rasmi wachezaji, jezi za timu na kujiandaa kwa msimu mpya, siku hii imekuwa maarufu kama Simba Day. 

Tangu ianzishwe imekua ikiboreka siku hadi siku, mwaka huu tumeona ni muhimu kuiboresha zaidi na hususan ukiangalia mchango wa timu yetu kwa jamii inayoizunguka.

Kuanzia mwaka jana Simba iliamua kuanzisha Simba Week ambayo lengo lake kuu ni kuwa wiki ya Simba Sports Club kufanya kazi za jamii, kukuza vipaji vya soka vya vijana, kutembelea wadau wa maendeleo na pia shughuli nyingine zenye tija kwa timu yetu na jamii kwa ujumla. 

Wiki hii itahitimishwa siku ya Simba Day ambapo mambo mengi mazuri yatafanyika. Kama ilivyokuwa mwaka jana, tutatengeneza program ambayo itawashirikisha wana Simba Nchi nzima. 

Tunategemea kuwa katika siku za kujitolea kwa jamii, wapenzi wote wa Simba Nchi nzima watajitokeza kufanya shughuli za kijamii kwenye maeneo yao. Simba inaamini kwa dhati tukiunganisha Nguvu zetu tunaweza kuleta madabiliko makubwa sana Nchini kwetu.

Ndugu wanahabari,
Habari njema leo ni nyingi na ubunifu ni jadi yetu. Napenda kuwataarifu rasmi kuwa siku ya Simba Day, Simba Sports Club itacheza mechi na Inter Clube ya Angola kwenye mechi hii wachezaji wetu wapya wataonekana rasmi baada ya maandalizi ya kutosha, kabla ya mechi hii kutakuwa na mechi kali ya utangulizi kati ya Simba Under 20 mechi hizi nina uhakika itakuwa burudani tosha.

Kama ambavyo mnajua Ubunifu ni jadi ya Simba tunatarajia kuwa na burudani mbalimbali, ikiwamo wimbo maalum wa Simba, Wanamuziki nguli na Surprise kwa watazamaji watakao lipia kiingilio.

Kama ilivyo kuwa mwaka jana Rais wa Simba atasaidiana na Kocha Mkuu wa Simba kwenye benchi la ufundi.

Ndugu wanahabari,
Kabla sijamaliza, napenda kuwashukuru sana kwa kuwa karibu na klabu yetu ya Simba.

Matukio ya hivi karibuni na yatakayo kuja katika siku chache zijazo yanatosha kuwaambia na kudhihirisha lengo na dhamira ya Uongozi wangu wa kujenga timu imara sio Tanzania tu, bali Afrika.

Nashukuru kwa kunisikiliza.

No comments:

Post a Comment