TANGAZO


Tuesday, March 22, 2016

Obama kukutana na upinzani Cuba

Rais wa Marekani Barack Obama amepangiwa kuhitimisha ziara yake ya siku tatu nchini Cuba kwa kukutana na wapinzani wa serikali.
Ameyapa kipaumbele masuala ya haki za kibinadamu na mageuzi ya kisiasa na kuyataja kuwa matakwa muhimu katika mashauriano yake na uongozi wa taifa hilo.
Alimwambia Rais Raul Castro katika kikao na wanahabari kwamba uhusiano baina ya nchi hizo mbili utanawiri tu iwapo raia watahakikishiwa uhuru wao nchini Cuba.
Wawili hao, kwenye kikao na wanahabari Jumatatu, walisema wanataka kushirikiana katika masuala yenye umuhimu kwa nchi zote mbili.
Bw Obama pia atatazama mechi maalum ya besiboli baina ya timu ya taifa ya Cuba na timu ya Tampa Bay Rays.
Gwaride Rais Castro na Rais Obama wakikagua gwaride la heshima
Rais Obama ndiye rais wa kwanza wa Marekani kuzuru Cuba akiwa bado uongozini katika kipindi cha miaka 88.

No comments:

Post a Comment