Mamlaka nchini Guinea imesema kuwa imewachunguza mamia ya watu ambao huenda wameambukizwa ugonjwa wa ebola baada ya mripuko mpya kuwaacha watu wanne wakiwa wamefariki kusini mashariki mwa taifa hilo.
Shirika la habari la Reuters limemnukuu msemaji wa kitengo kinachokabiliana na ugonjwa huo aliyekuwa akizungumza katika runinga moja akisema kuwa takriban watu 816 kutoka familia 806 tangu Jumamosi wametambuliwa kwamba huenda walishikana na waathiriwa.
Amesema kwamba watawekwa katika karantini kwa wiki tatu.
Ebola Guinea
Zaidi ya watu 11,000 walifariki kutokana na ugonjwa huo nchini Guinea,Liberia na Sierra Leone ambao ulianza mwaka 2013.
Mataifa yote matatu yameshuhudiwa visa vichache vya ugonjwa huo tangu udhibitiwe.
No comments:
Post a Comment