TANGAZO


Tuesday, March 22, 2016

Tenisi:Mwandalizi wa Indian Wells ajiuzulu kwa ''matamshi'' yake

   Raymond Moore

Mkurugenzi mkuu wa maandalizi ya michuano ya tenisi huko Indian Wells Raymond Moore amejiuzulu baada ya matamshi yake yaliozua utata kuhusu wanawake katika mchezo huo.
Mchezaji nambari moja duniani kwa upande wa wanawake Serena Williams alisema kuwa matamshi ya Moore yana kera na yasio ya ukweli.
Lakini mwenzake kwa upande wa wanaume Novak Djokovic alidai kuwa ziara yake inafaa kupigania wanaume wapewe fedha zaidi.
Serana Williams
Moore alisema kuwa wachezaji wanawake wanafaa kuwapigia magoti wenzao wa kiume kama vile Roger Federer na Rafael Nadal.
Lakini mchezaji huyo wa zamani wa Afrika Kusini baadaye aliomba msamaha kwa matamshi yake.
Gwiji wa mchezo huo Martina Navratilova alisema kwamba matamshi ya Moore yanachukiza sana,akiongezea kuwa wachezaji wanawake huenda wakasusia michuano ya Indian Wells iwapo Moore ataendelea kuwa mwandalizi.
Novak Djokovic
Djokovic ambaye alishinda taji la BNP la Paribas Open huko India Wells siku ya Jumapili aliyaelezea matamshi ya Moore kama yasio sawa.
Lakini raia huyo wa Serbia mwenye umri wa miaka 28 alihoji kwamba wanaume wanafaa kupewa fedha zaidi kwa sababu watu wengi huangalia mechi zao.

No comments:

Post a Comment