Maafisa wa polisi nchini Uganda wamekabiliana na wafuasi wa upinzani mapema siku ya Jumanne baada ya kutotolewa kwa uamuzi kuhusu kifungo cha nyumbani anachohudumu kiongozi wa upinzani Kizza Besigye.
Wafuasi wa bwana Besigye walikongamana nje ya mahakama karibu na Kasangati huko Kampala mapema leo.
Image caption
Maafisa wa usalama wasambazwa kukabiliana na wafuasi wa upinzani
Walitarajia kutolewa kwa uamuzi huo katika kesi iliowasilishwa na mawakili wake kufuatia ombi la mkurugenzi wa mashtaka.
Nje ya mahakama wakili wa Besigye David Mpanga alisema kuwa kasi ya vile faili ya kesi hiyo ilivyorudishwa inatia wasiwasi.
Maafisa wa polisi wakikabiliana na wafuasi wa upinzani nchini Uganda
Wafuasi waliapa kuelekea hadi katika nyumba ya Besgye kabla ya polisi kupelekwa.
No comments:
Post a Comment