TANGAZO


Tuesday, March 22, 2016

Wengi wauawa katika mashambulio Brussels

Moshi Moshi umeonekana ukitoka kwenye moja ya majumba katika uwanja huo
Milipuko imetokea katika uwanja wa ndege wa Zaventem na kituo cha treni cha Maelbeek mjini Brussels na kuua watu wengi.
Msemaji wa wazimamoto mjini Brussels Pierre Meys amenukuliwa na shirika la habari la AFP akisema watu 21 wamefariki katika mashambulio hayo mawili, uwanja wa ndege na kituo cha treni.
Amesema watu 11 walifariki katika milipuko iliyotokea uwanja wa ndege.
Kampuni inayosimamia uchukuzi wa treni Brussels imesema kwamba watu 15 walifariki Maelbeek na wengine 55 kujeruhiwa.
Watu wameondolewa kutoka kwenye uwanja huo na safari za ndege kutua au kupaa kutoka uwanja huo kukatizwa.
Waziri Mkuu wa Ufaransa Francois Hollande amelaani mashambulio hayo mjini Brussels na kusema ni kama mashambulio yaliyolenga bara lote la Ulaya.
Waziri Mkuu wa Ubelgiji Charles Michel amesema hatua zaidi zimechukuliwa kuimarisha usalama mpakani.
Vyombo vya habari nchini Brussels vinaripoti kwamba milipuko ilitokea karibu na meza ya shirika la ndege la American Airlines.
Haijabainika ni nini chanzo cha milipuko hiyo.
Milipuko pia imeripotiwa katika kituo cha treni cha Maelbeek karibu na majengo taasisi za Umoja wa Ulaya. Mfumo wa uchukuzi wa treni mjini Brussels umefungwa.
Milipuko hiyo imetokea siku nne tu baada ya kukamatwa kwa mshukiwa mkuu wa mashambulio ya Paris ya mwaka jana ambayo yalisababisha vifo vya watu 130.
Abdeslam alikamatwa Ijumaa katika mtaa mmoja wa Brussels.
Uwanja wa ndege wa Zaventem unapatikana kilomita 11 kaskazini mashariki mwa Brussels na ulihudumia abiria zaidi ya 23 milioni mwaka jana.

No comments:

Post a Comment