TANGAZO


Saturday, March 19, 2016

Mshukiwa mkuu wa shambulio la Paris akamatwa

Maafisa wa polisi nchini Ubelgiji wakimkamata mshukiwa

Rais wa Ufaransa Francois Hollande ameonya kuwa mitandao ya kigaidi barani Ulaya inaendelea kuimarika licha ya kukamatwa kwa mmoja wa washukiwa wa mashambulizi ya mwezi Novemba mjini Paris.
Eneo lililovamiwa na maafisa wa polisi
Mtu mwingine ambaye pia anashukiwa kuhusika kwenye mashambulizi hayo ya mwezi Novemba alijeruhiwa na kukamatwa na kwa ujumla watu watano walikamatwa.
Maafisa wa polisi
Bwana Hollande alisema kuwa vita havitakwisha hadi kila mmoja aliyehusika kwenye shambulizi la Paris akamatwe. Watu 130 waliuawa wakati wa shambulizi hilo.

No comments:

Post a Comment