TANGAZO


Saturday, March 19, 2016

Makombora:UN yaishtumu Korea Kaskazini


 
Korea Kaskazini
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeishutumu vikali Korea Kaskazini kufuatia majaribio ya hivi majuzi ya makombora ya masafa marefu na kuitaka iache kukiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa.
Siku ya Ijumaa Korea Kaskazini ilirusha kombora moja ambalo lilisafiri karibu umbali wa kilomita 800 kabla ya kuanguka baharini
Pia ilirusha makombora mawili ya masafa mafupi mapema mwezi huu.

No comments:

Post a Comment