TANGAZO


Tuesday, March 29, 2016

BUNGE LA TANZANIA: TAARIFA KWA UMMA

Katika kutekeleza majukumu yake, Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo imepanga kufanya mikutano ya kusikiliza maoni ya wadau (Public Hearing) kwa mujibu wa Kanuni ya 117 (9) kuhusiana na Sheria Ndogo zilizowasilishwa na Serikali katika Mkutano wa Pili wa Bunge uliomalizika Februari 2016. 

Mikutano hiyo ya kusikiliza maoni ya wadau kuhusu Sheria Ndogo inatarajiwa kufanyika Jumatatu tarehe 4 Aprili, 2016 na Jumanne tarehe 5 Aprili, 2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam. 

Sheria Ndogo ambazo Kamati inakaribisha wadau na umma kwa ujumla kutoa maoni yao ni pamoja na zifuatazo:- 

1. The Petroleum (Bulk Procurement) Regulations, 2015 
2. The Public Private Partnership Regulations, 2015 
3. The Copyright and Neighboring Rights (Copyrighted Works - Communication to the Public) Regulations, 2015 
4. The National Examinations Regulations, 2015 
5. The Institute of Judicial Administration Lushoto (Students’ General Welfare, Conduct and Disciplinary Matters) Regulations, 2015 
6. The Institute of Judicial Administration Lushoto (Students’ Performance Assessment) Regulations, 2015 
7. The Fire and Rescue Force (Fire Precautions in Buildings) Regulations, 2015 

Sheria Ndogo zilizotajwa hapo juu pamoja na nyingine ambazo zinashughulikiwa na Kamati, zinapatikana kwa kupakua (downloadable) katika tovuti ya Bunge la Tanzania ya www.parliament.go.tz pamoja na tovuti ya Serikali ya www.tanzania.go.tz 

Aidha, maoni ya wadau yanaweza kuwasilishwa kwa njia ya posta au barua pepe kwa anuani ifuatayo:- 
Katibu wa Bunge, Ofisi ya Bunge, S. L. P. 9133, DAR ES SALAAM 
Barua pepe: cna@bunge.go.tz 

Imetolewa na: Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano Ofisi ya Bunge DAR ES SALAAM 29 Machi, 2016.

No comments:

Post a Comment