TANGAZO


Tuesday, December 1, 2015

Tigo yafikisha upatikanaji wa huduma ya 4G LTE Dodoma

Mkuregenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) katika uzinduzi wa huduma ya 4G LTE jijini Dodoma, kushoto ni Meneja wa huduma ya 4G LTE, Benedict Mponzi.
Mkurugenzi wa kanda ya Kaskazini kutoka Tigo Bw.George Lugata akimkabidhi Bw.Danson Kaijage kushoto laini mpya ya 4G LTE katika uzinduzi wa huduma ya 4G LTE, katikati ni Territory Meneja wa Dodoma, Singida na Kondoa Bw.Innocent Anthony kutoka Tigo jijini Dodoma.

*Ni baada ya kuanza kutoa huduma hiyo kwa 
ufanisi jijini Dar es Salaam

Dodoma, Novemba 30 2015. 
WATEJA wa Tigo waishio Dodoma sasa wanaweza 
kupata mtandao wa intaneti wenye kasi kubwa zaidi kufuatia upanuzi wa upatikanaji wa huduma ya 4G LTE hadi kufikia jiji hilo lilopo kaskazini mwa Tanzania Teknolojia ya 4G LTE ina kasi mara tano zaidi kuliko teknolojia ya 3G inayopatikana nchini kwa sasa.


"Upanuzi huu umetokana na mafanikio makubwa
yaliyopatikana katika majaribio ya awali ya utoaji huduma ya 4G jijini Dar es Salaam kuanzia mapema mwaka huu’’, amesema Mkurugenzi wa kanda ya Kaskazini, George Lugata.

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini 
Dodoma, Lugata amesema: "ni kielelezo cha jinsi 
ambavyo Tigo imedhamiria kufanikisha kuleta 
mabadiliko ya dijitali katika maisha ya watanzania
na pia kuwa katika msitari wa mbele wa kutumia 
teknolojia ya kisasa na kibunifu nchini Tanzania."

Mtandao wa 4G LTE una kasi kubwa zaidi katika 
kuperuzi na kupakua kwa rahisi kutoka kwenye 
mtandao wa intaneti na pia katika kufanya 
mawasiliano kwa njia ya Skype. Huduma hii pia
inaharakisha urushwaji wa picha za video na ubora
hali ya juu na kufanya mikutano kwa njia ya 
mtandao.

“Tunapenda kuwahakikishia wateja wetu waishio 
Dodoma kwamba sasa wanaweza kufurahia huduma 
bora zaidi za mawasiliano kutoka Tigo na Intaneti 
yenye kasi zaidi,” Lugata amesema. Dodoma ni 
moja wapo ya miji mikubwa Tanzania, na pia 
inajivunia Bunge la Tanzania na kwa sababu ya 
kuwa na vyuo viwili vikubwa Tanzania.

Wateja wote wa Tigo 4G LTE watanufaika na 
promosheni; kila atakapo ongeza salió la shilingi  
elfu moja au zaidi, atapata mb 500 bure kama bonasí.

Ametaja miji mingine katika mikoa sita ambapo 4G 
itaanza kupatikana hivi karibuni kuwa ni, Morogoro, 
Moshi, Mwanza na Arusha,Tanga na hapa Dodoma 
“jambo ambalo linaifanya Tigo kuwa na mtandao 
mkubwa wa 4G nchini Tanzania.” 

Lengo kuu ni kufikisha huduma ya 4G katika kila 
kona za nchi ifikapo mwaka ujao, Lugata ameongeza kusema.

No comments:

Post a Comment