TANGAZO


Tuesday, December 1, 2015

Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi afanya ziara TRL

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Bw. Shabani Mwinjaka akiongea na waandishi wa habari alipofanya ziara yake katika shirika la reli Tanzania (TRL) leo jijini Dar es Salaam. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Bw. Shabani Mwinjaka akienda kukagua moja ya karakana za shirika la reli Tanzania (TRL)  alipofanya ziara yake Tanzania leo jijini Dar es Salaam. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Bw. Shabani Mwinjaka akitoka kukagua moja ya karakana za shirika la reli Tanzania (TRL), alipofanya ziara yake Tanzania leo jijini Dar es Salaam. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Bw. Shabani Mwinjaka akikagua moja ya karakana za shirika la reli Tanzania(TRL)  alipofanya ziara yake Tanzania leo jijini Dar es Salaam. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Bw. Shabani Mwinjaka akisisistiza jambo kwa wafanyakazi wa shirika la reli Tanzania(TRL)  alipofanya ziara yake Tanzania leo jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Ally Daud - Maelezo)

Na Ally Daud-Maelezo
Dar es Salaam
30/12/2015
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi  Shabani Mwinjaka amefanya ziara katika Shirika la Reli Tanzania (TRL)ili kuhakikisha ufanyaji kazi wa shirika hilo linaendana na kasi yaRais wa awamu ya tano Mh.  John Pombe Magufuli.

Katika ziara hiyo Bw. Mwinjuko alikagua karakana za shirika hilo ili kuona utendaji wake na kusisitiza ukarabati wa mebehewa yaliyobaki kumaliziwa ndani ya siku 30.

Hata hivyo katibu  huyo amestushwa na habari ya kuanguka kwa mabehewa 50  ya mafuta  yaliyokuwa yanajaribiwa  huko Tanga.

“Nimestushwa na taarifa ya kuanguka kwa mabehewa 50 ya mafuta katika majaribio baada ya kujazwa maji ,yangekuwa yana mafuta ingekua hasara kubwa kwa Tanzania hivyo nataka tatizo hilo lishughulikiwe haraka iwezekanavyo kunusuru mabehewa yaliyobaki .”alisema Mwinjaka.

Mbali na hayo Bw.Mwinjaka alisema kwamba reli ambazo zimehifadhiwa katika karakana hizo ziondolewe na zikamalizie ujenzi wa reli ambazo hazijaisha kuliko kukaa  bila ya matumizi huku kukiwa na shida ya mataaluma hayo.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania Bw.Elias Mshana amesema kwamba wapo katika mchakato wa kumalizizia ukarabati wa mabehewa yaliyobaki pamoja na marekebisho ya reli zilizoharibika na mpaka 31 Desemba mwaka huu zitakua zimetengemaa.


“Tunatarajia mpaka tarehe 31 Decemba mwaka huu tutakua tumemaliza kukarabati mabehewa na reli zilizoharibika ili zianze kutumiwa rasmi ili kuleta maendeleo katika Nchi” Alisema Bw. Mshana.

No comments:

Post a Comment