Baadhi ya wanafunzi wa Kitanzania wanaojifunza lugha ya Kichina katika kituo cha Utamaduni wa China nchini Tanzania wakiimba nyimbo kwa lugha ya Kichina mbele ya mgeni rasmi Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (hayupo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa kituo hicho.
Kundi la Muziki la Zinijncheng kutoka chuo Kikuu cha Sanaa ya Muziki cha China kikitoa burudani kwa mgeni rasmi Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (hayupo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa kituo cha Utamaduni wa China nchini Tanzania.
Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (katikati) akipata maelekezo toka kwa Mshauri wa Masuala ya Utamaduni toka Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China Bw. GAO Wei (kulia) wakati Waziri Mkuu akifungua kituo cha Utamaduni wa China nchini Tanzaniamapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel.
Mshauri wa Masuala ya
Utamaduni toka Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China Bw. GAO Wei akitoa ufafanuzi
wa picha za matukio mbalimbali kwa Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (katikati)
mara baada ya Waziri Mkuu Mstaafu kufungua kituo cha utamaduni wa China nchini
Tanzania mapema hii leo jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Eliphace Marwa - Maelezo)
No comments:
Post a Comment