TANGAZO


Wednesday, December 16, 2015

Benki ya NMB yazindua mfumo wa kisasa wa utunzaji wa taarifa za mikopo, wateja sasa kupata mikopo ndani ya siku 4


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu mfumo wa kisasa wa utunzaji wa taarifa za mikopo uliozinduliwa na Benki hiyo. Mfumo huo utatutumika kwenye kanzi data ya Mikopo ya Benki hiyo (CRB's) na kuwawezesha wateja wakubwa na wadogo wa wanaoomba mikopo kutoka NMB kuipata ndani ya siku 1 hadi 4 kutokana na taarifa zao za mikopo kuendelea kuwepo kwenye mfumo wa Benki hiyo.

Ofisa Mkuu Udhibiti wa Hasara wa Benki ya NMB Bw. Tom Borghols (wa pili kutoka kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) namna Benki ya NMB  inavyoongoza katika utoaji wa mikopo kwa makundi mbalimbali.

Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Wadogo wa Benki ya NMB Bw. Abbdulmajid Nsekela (kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu kuanzishwa kwa mfumo wa kisasa wa utunzaji wa taarifa za mikopo kwa wateja uliozinduliwa na Benki ya NMB na jinsi utakavyoongeza ufanisi kwa kuwawezesha wateja kupata mikopo kwa haraka. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc Ineke Bussemaker . 

No comments:

Post a Comment