Na Skolastika Tweneshe na Tupokigwe Marco.
WAZEE wa shirikisho la filamu Tanzania (TAFF)
hawajakubaliana na uamuzi wa Rais
wa shirikisho hilo Bw. Simon Mwakifwamba kutogombea
tena nafasi ya Uraisi katika shirikisho hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini
Dar es Salaam, Msemaji wa wazee wa Shirikisho
hilo Bw. Ahmed Olotu maarufu kama Mzee
Chilo amesema kuwa wao kama Wazee wakongwe katika Shirikisho hilo wamemuomba Rais
huyo agombee tena wadhifa huo kwa mara nyingine ili aweze kumalizia
mambo muhimu ya maendeleo katika tasnia ya sanaa.
“Sisi kama wasanii na Wazee wakongwe katika tasnia
hii, bila kushurutishwa na mtu yeyote tunapinga uamuzi wake wakutotaka kugombea tena
nafafasi hiyo .” Alisema Olotu.
Aidha,
ameongeza kuwa, miradi kama TAFF Trust
Fund, TAFF Creative Ltd na mingine mingi yenye kuhitaji umakini ambayo
imehasisiwa chini uongozi wake inahitajika kumaliziwa kwani bado haijakamilika.
Kwa
upande wake Bi. Salome Nonge (Mama Abdul)
ameeleza kuwa, Bwana Mwakifwamba ndiye aliyesaidia kupatikana kwa Ofisi ya Wasanii pamoja na
usafiri katika kazi
zao.
“Binadamu
hakosi kasoro ila kwa Mwakifwamba ni
ndogo mno sasa hatutaki mtu mwingine
aje.”Bi Salome alisema.
Naye
Bi. Salumu Ally (Mkasi) ameeleza kuwa uongozi
wa Mwakifwamba umesaidia wasanii kupata
haki zao kama hati miliki zilizowezesha kupata maendeleo ya kiuchumi
kupitia sanaa wanaoifanya.
Hata
hivyo sanaa ya filamu inakuwa kwa kasi nchini pamoja na changamoto zilizopo ambapo
juhudi katika kutengeneza kazi zenye ubora zitakazoleta ushindani katika soko
la kitaifa na kimataifa bado zinahitajika.
No comments:
Post a Comment