Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Donan Mmbando (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi wakati akipokea msaada huo kutoka WHO. Kulia ni Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Nchini Dk. Rufaro Chatora.
Taarifa ikitolewa kabla ya kupokea msaada huo.
Hapa wakitiliana saini mkataba wa kupokea msaada huo.
Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Nchini Dk. Rufaro Chatora (katikati), akimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Donan Mmbando (kushoto), dawa ya maji zenye thamani ya sh. milioni 42.2 zilizotolewa na WHO kwa ajili ya kusaidia kukabiliana na magonjwa ya mlipuko nchini, Dar es Salaam leo asubuhi. Anayeshuhudia tukio hilo kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Uhakiki na Ubora wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Mohamed Ali Mohamed.
Na Dotto Mwaibale
SERIKALI imepokea msaada wa dawa ya kutakasa maji ya Waterguard kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO),kwa lengo la kukabiliana na magonjwa ya mlipuko zenye thamani ya sh. milioni 42.
Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi mara baada ya kupokea dawa hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mmbando, alisema dawa hizo ni waterguard cotton (1000) na Cresol Saponated Liquid (100) litres ambayo itasaidia kutakasa maji ili kuepusha magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu.
Alisema dawa hiyo itasaidia kudhibiti ugonjwa huo kwani kila siku zinavyozidi kwenda wagonjwa wanazidi kuongezeka hivyo dawa hiyo itatumika kupunguza maambukizi mapya.
"Hali ya mazingira bado hairidhishi idadi ya wagonjwa inazidi kuongezeka hadi sasa, tangu ugonjwa uanze kuripotiwa wagonjwa walioripotiwa kwa Dar es salaam ni 385 na vifo vya watu 8," alisema.
Alitaja mgawanyiko wa wagonjwa katika kila manispaa Kinondoni 292 , Ilala 60 na Temeke 33, aliongeza idadi ya wagonjwa waliopo kwenye kambi za matibabu hadi Agosti 27, jumla ni 74 ambapo kituo cha Mburahati 53 , Buguruni ikiwa na wagonjwa 14 huku Temeke 7.
"Kwa Mkoa wa Morogoro idadi ya wagonjwa hadi Agosti 28, wagonjwa 60 na walioko kambini ni 9 na kifo 1...moja ya sababu ambazo zinachangia kuendelea kua na ugonjwa huu hapa nchini ni kunywa maji yasiyo safi na salama,"alisema.
Mmbando alitoa tahadhali kwa wananchi kujizuia kunywa maji yasiyo safi na salama,kuepuka kula chakula kilichopoa au kuandaliwa katika mazingira yasiyo safi hali hiyo itasaidia kutokomeza ugonjwa huo na kuwataka kuchemsha maji ya kunywa na kuweka dawa.
Akikabidhi msaada huo Mwakilishi Shirika la afya duniani (WHO), Dk. Rufaro Chatora alisema anamini dawa hizo zitasaidia kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.
"Msaada huu tuliyotoa utasaidia wananchi kwa kiasi kikubwa katika kupunguza maambukizo mapya ya ugonjwa huu ambao huwa unaua kwa kiasi kikubwa,"alisema. (Imeandaliwa na Dotto Mwaibale)
No comments:
Post a Comment