TANGAZO


Monday, August 17, 2015

Washiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 wajipatia kipato kwa kuuza bidhaa walizotengeneza katika Kijiji cha Kisanga

NI siku ya 14 ambapo mampema kabisa washiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula Msimu wa nne 2015 linaloendeshwa na Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow na yenye kauli yake ya Wekeza kwa wakulima wadogo wadogo wanawake inalipa , na Kipindi ambacho kinaruka katika Runinga yako kupitia Chanel ya ITV kuanzia saa 12:30 jioni na Marudio saa 11:30 za asubuhi , Katika siku hii Mama Shujaa wa Chakula wanatoka na kuelekea mabondeni kufuata udongo wa Mfinyanzi kwa ajili ya kuja kutengeneza vitu mbalimbali kama majiko, Mifuniko, Mabanda, mapambo, Vyungu na vitu vyengine vingi. 

Ilikuwa ni Safari ndefu ya kufuata udongo huo lakini hatimaye walifanikiwa kuupata na baadae kurudi katika Kijiji chao cha Kisanga na kuanza kutengeneza vitu hivyo na baadae kuwauzia wanakijiji wa Kijiji cha Kisanga.

Pia hii ilikuwa ni nafasi kubwa na ya kipekee kwa Washiriki hao wa Shindano la mama Shujaa wa Chakula kuuza vitu vyao ambavyo walitengeneza wakiwa kwao pamoja na Bidhaa mbalimbali kwa wakazi wa Kijiji cha Kisanga... Hivi ndivyo ilivyokuwa.
Mama Shujaa wa Chakula wakiwa wanaelekea Bondeni katika kijiji cha Kisanga kufuata udongo wa Mfinyanzi kwa ajili ya kutengeneza vitu mbalimbali ambavyo viliwasaidia kupata kipato.
Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula Msimu wa nne 2015 Shindano linalo endeshwa na Oxfam kupitia Kampeni yake ya Grow wakiwa wanachimba udongo wa Mfinyanzi kwa ajili ya kwenda kutengeneza vitu mbalimbali ambavyo baadae waliviuza.
Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 msimu wa nne wakiwa wanamalizia kuchimba udongo.
Kazi imeanza ambapo washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa chakula linalo endeshwa na Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow na Kurushwa katika Runinga yako kupitia Chanel ya ITV kuanzia saa 12:30 za jioni na Kurudiwa saa 11:30 asubuhi wakiwa bize kila mtu kufinyanga vitu mbalimbali.
Kila mmoja yupo bize kutengeneza kitu chake.
Kazi inaendelea ambapo mmoja wa washiriki anaonekana akitengeneza kitu chake kwa ustadi mkubwa.
Hiki kikiwa katika hatua za mwisho.
Mmoja wa washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015 akiwa anamalizia kutengeneza kitu chake kwa umakini Mkubwa.
Wakiendelea kufinyanga vyungu.
Wakiendelea kukamilisha kutengeneza vyungu pamoja na Majiko kwa kutumia udongo wa mfinyanzi.
Sasa kila kitu kimekamilika washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015 wakiwa  wameweka bidhaa zao ambazo wamezitengeneza kijijini pale na zengine wametoka nazo makwao kwa ajili ya kuziuza kwa wanakijiji wa Kisanga. 
Baadhi ya wanakijiji wa kijiji cha Kisanga   wakiwa wamefika katika sehemu ambayo akina mama shujaa wa chakula walikuwa wanauza vitu vyao ambavyo walitengeneza kijijini hapo na vyengine walitoka navyo makwao na  kuvinunua.

No comments:

Post a Comment