TANGAZO


Friday, August 14, 2015

Wahamiaji 100 kutoka Asia wanaswa Uganda

Wahamiaji kutoka Asia waliokamatwa Urusi, wahamiaji wengine 100 wamekamatwa Uganda

Polisi nchini Uganda inamshikilia mshukiwa mmoja na kumsaka mwingine katika kile kinachoonekana kama kusafirisha watu kinyume na sheria.
Aidha wanajiandaa kuwarejesha makwao wahamiaji 30 kati ya 100 waliokamatwa.
Kuna raia zaidi ya 100 kutoka bara hindi ambao wako mjini Kampala wakidai walihadaiwa na tapeli mmoja aliewaahidi kuwapa ajira nchini Afrika Kusini lakini mtu huyo hajulikani mahali alipo.
Polisi hao wanasema huenda kukawa mtandao wa watu wanaosafirisha kimagendo watu kutoka nje ya nchi kuwaleta hapa na pia kuwapeleka kwingineko kwa visingizio vya kuwapatia ajira kinyume na utaratibu ulioko.
Hii inatokana na taarifa kuwa raia zaidi ya 20 kutoka bara hindi wamekuwa katika mahote limbalimbali mjini Kampala wakisubiri kupelekwa nje
Raia hao kutoka bara hindi waliingia Uganda kama watalii lakini aliewaleta akatoweka na hivyo kubaki wakichanganyikiwa bila pesa za kulipia chakula na malazi.
Binoga Moses ni kamishna wa polisi anaehusika na kitengo kinachopigana dhidi ya kuwasafirisha kimagendo wanadamu.
'Tulipohoji hawa wahindi 29 walitwambia kuwa idadi ya walioletwa Uganda kwa njia hizo ni zaidi ya 100.Lakini hadi sasa tumewatambua hao 29.'
Maafisa a uhamiaji walifichua mapema wiki hii kuwa washukiwa wawili-mkiwemo mmoja anaeitwa Domalia Jayesh,akitumia jina la kupanga la Vijay Shamia, aliwa hadaa wahindi hao kuwa atawasaidia kupata kazi nchini Afrika Kusini kwa gharama ya dola elf mbili na mia tano kila mmoja.
Afisa polisi Binoga ameongeza kuwa mshukiwa Jayesh anasemekana kuwapatia vyumba vya kulala wahindi hao katika hoteli mbalimbali ambazo amekataa kuzitaja-miezi miwili iliopita.


Lakini tangu hapo hajulikani aliko huyo mshukiwa.Mke wa mshukiwa huyo anashikiliwa na polisi katika kituo cha polisi mtaa wa Kabalagala –hapa Kampala-kama mshukiwa mkuu.
Hii sio ara ya kwanza raia kutoka bara hindi wakikwama Uganda katika kile kinachoonekana kama biashara ya watu hao.Bwana Binoga wa polisi anaeleza.
'Wiki mbili zilizopita raia 21 kutoka Bangladesh nao walikwana katika hoteli hapa baada ya kuletwa hapa na raia mmoja wa Bangladesh. Walikuwa wameahidiwa kupelekwa Sudan Kusini; Sudan ya Khartoum na Afrika Kusini ili kuweza kupewa ajira.'
Polisi inasema visa kama hivyo vimeongezeka siku hizi bila kutoa sababu.
Aidha huenda ile viza moja ya utalii inayozijumulisha Kenya Uganda na Rwanda ndio imechochea hali hiyo.
Ripoti ya kila mwaka kuhusu makossa ya kusafirisha watu kimagendo,yam waka jana ilionyesha kuwa Uganda ilikuwa na kesi hizo 105.Idadi hii inaonekana kama ndogo kuliko ile ya mwaka wa 2013 ilioonyesha kesi kuwa 154.
Labda kupungua huko kumesababishwa na hatua ya vikosi vya dola kuwa macho.
Duru maalum zinazonukuu wizara ya mambo ya nje ya marekani zinasema kuwa kila mwaka binadamu walio kati ya laki sita na nane husafirishwa kimaendo duniani kote na kati ya hao asili mia 80 ni wanawake ilhali nusu yao ni watoto.

No comments:

Post a Comment