Serikali ya Kenya imeharibu boti moja iliyopatikana imebeba takriban kilo 7 za mihadarati aina ya Heroini.
Boti hiyo inayoitwa 'Baby Iris' ilikamatwa na polisi kwa tuhuma za ulanguzi wa mihadarati.
Ripoti ya polisi inasema kuwa 'Baby Iris' inamilikiwa na bwenyenye mmoja raia wa Uingereza.
Boti hiyo iliyokamatwa katika bahari ya Kenya huko Mombasa itaharibiwa kuambatana na sheria za Kenya.
Jeshi la wanamaji la Kenya ndilo lililokabidhiwa jukumu hilo la kuiharibu boti hilo Na walitekeleza wajibu wao kwa uadilifu kwa kuifunga vilipuzi kisha kuipeleka eneo la mbali katika Bahari hidi kisha kuilipua.
Mwandhishi wetu aliyeko huko Ferdinand Omondi anasema kuwa boti hiyo ilikuwatayari imeshaharibiwa kwa mabomu katika eneo karibu na Mombasa pwani ya Kenya .
No comments:
Post a Comment