TANGAZO


Friday, August 14, 2015

Wachimbaji wadogo wa madini Chunya wanolewa kuhusu OMCTP

Baadhi ya wachimbaji wadogo wa Madini wa Wilayani Chunya wakifuatilia kwa makini mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini. 
Ofisa Madini Mkazi- Chunya, Mhandisi Donald Mremi akifunguwa mafunzo kuhusu Mfumo wa Huduma ya Leseni kwa Njia ya Mtandao kwa wachimbaji wadogo, wilayani Chunya.  
Baadhi ya Wachimbaji wadogo wa Madini waliohudhuria mafunzo hayo wakimsikiliza Mtaalamu (hayupo pichani).
Maofisa kutoka Ofisi ya Madini ya Ofisa Mkazi- Chunya wakifuatilia mafunzo. Wa kwanza kushoto ni Samwel Gombekile, Mzee Mussa (katikati) na Severine Haule. 
Baadhi ya Wachimbaji wadogo wa Madini waliohudhuria mafunzo hayo wakimsikiliza Mtaalamu (hayupo pichani). 
Mtaalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Idd Mganga akiendelea na mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa Madini wilayani Chunya.

Na Mohamed Seif, Nishati na Madini
Wachimbaji wadogo wa madini nchini wametakiwa kutohofia Mfumo wa Huduma ya Utoaji Leseni kwa njia ya Mtandao ujulikanao kama Online Mining Cadastre Transactional Portal (OMCTP).

Wito huo umetolewa leo (14/08/2015) wilayani Chunya na Ofisa Madini Mkazi- Chunya, Mhandisi Donald Mremi wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Huduma ya Leseni kwa wachimbaji Madini wa wilayani hapo. 

Mhandisi Mremi alisema Mfumo huo wa kielektroniki ni rafiki kwa mtumiaji na hivyo kuwataka wachimbaji madini nchini wasiogope na badala yake wasikilize kwa makini mafunzo yanayoendelea kutolewa na wataalamu wa Wizara hiyo ikiwa ni pamoja na kuzingatia watakayoelezwa.

“Nawaomba msikilize kwa umakini yale ambayo wataalamu wataeleza na pia baada ya mafunzo mfike Ofisini ili tuwasajili na pia tutaendelea kuwa tunawapatia mafunzo kuhusu huduma hii,” alisema Mremi.

Wizara ya Nishati na Madini ilizindua mfumo wa Huduma za Leseni kwa njia ya mtandao tarehe 8 Juni, 2015. Pamoja na malengo mengine, Mfumo huo umeanzishwa ili kutekeleza agizo la Serikali la kutaka Wizara na taasisi za Serikali ziwe zinapokea malipo ya Serikali kwa njia za kielektroniki. 

No comments:

Post a Comment