TANGAZO


Saturday, August 22, 2015

Tamasha la kuombea Uchaguzi Mkuu kuanzia Dar Oktoba 4


Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo kuhusu kukamilika kwa maandalizi wa Tamasha la Injili la kuombea amani Tanzania kuelekea Uchaguzi Mkuu, katika Mikoa 10, ikiwemo Dar es Salaam litalofanyika Oktoba 4, mwaka huu. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com) 
Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama akifafanua jambo, wakati alipozungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo kuhusu kukamilika kwa maandalizi wa Tamasha la Injili la kuombea amani Tanzania kuelekea Uchaguzi Mkuu, katika Mikoa 10, ikiwemo Dar es Salaam litalofanyika Oktoba 4, mwaka huu. 
Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama akielezea kuhusu tamasha hilo. 

Mwandishi wetu
MATAMASHA ya kuombea amani na utulivu katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu nchini, yataanzia Dar es Salaam Oktoba 4, kwenye Uwanja wa Taifa.

Akizungumza leo, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama alisema matamasha hayo yatafanyika kwenye mikoa 10, huku akitaja mitano ya awali ambapo wasanii wataombea amani kupitia muziki wa Injili utakaoporomoshwa na waimbaji mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.

Aliitaja baadhi ya mikoa itakayofanyika tamasha hilo ni Dar es Salaam, Morogoro, Iringa, Mbeya Shinyanga na Mwanza.

Msama alisema, tamasha la kwanza lenye dhamira hiyo litafanyika Oktoba 4 jijini Dar es Salaam.

"Tumeona kuna umuhimu kuwashirikisha waimbaji wa nyimbo za Injili kumuomba Mungu wakati tukielekea kwenye uchaguzi, wakati wa kampeni kuna vyama vyanye itikadi mbalimbali lakini kuna umuhimu wa kuwepo amani na watanzania tuendelee kuwa wamoja," alisema Msama.

Alisema kuna umuhimu mkubwa kumwomba Mungu kwa sala, nyimbo na kumtukuza ili uchaguzi Mkuu ufanyika kwa amani huru na haki.

Alisema tamasha hilo litakalokuwa na kauli mbiu ya 'Tanzania ni ya kwetu Tulinde, na kuitunza Amani ya Nchi Yetu litajumuisha waimbaji wa muziki wa injili wa ndani na nje ya nchi ikiwemo za Rwanda, Kenya na Uganda watakaosaidia kumwomba Mungu.

Aliwataja baadhi ya waimbaji ambao wamethibitisha kushiriki katika tamasha hilo ni Bonny Mwaitege na  Christopher Muhagaira.

Mjumbe wa kamati ya tamasha hilo, Hamis Pembe alisema maandalizi ya tamasha hilo yanaendelea vizuri, pamoja na kuimba nyimbo zao zenye ujumbe wa amani na upendo lakini pia wataimba wimbo wa pamoja.

Alisema kuelekea katika uchaguzi huo matamasha hayo wanatarajia kuwepo matukio mengine kama ya kumuaga Rais anayemaliza muda wake, Jakaya Kikwete.

Msama aliwataka wananchi kujiandaa kupata ujumbe wa kudumisha amani na utulivu kwa kumwomba Mungu kupitia nyimbo katika tamasha hilo, anaamini atasikia.

No comments:

Post a Comment